Exclusive: Babu Seya Alivyofunga Ndoa Kanisa La Sinza Dar (Picha +Video)
MWANAMUZIKI mkongwe Nguza Viking almaarufu Babu Seya jana Septemba 7, 2019 amefunga ndoa na Bi Desderia Philip Haule katika Kanisa Takatifu Katoliki Parokia ya Bikira Maria, Sinza, jijini Dar es Salaam na kumalizia furaha hiyo kwenye sherehe iliyofanyika Hoteli ya Landmark iliyopo Mbezi Beach jijini ambapo wageni waalikwa walifaidi vyakutosha.
Ndoa ya Babu Seya na mkewe imefungwa na Paroko wa Kanisa Takatifu Katoliki Parokia ya Bikira Maria, Sinza, Cuthbert Maganga.
PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL
Comments are closed.