EXCLUSIVE: FAMILIA inayoishi kwenye pango zaidi ya miaka minane, hapa ni nyumbani kwa Nuru Lugina, almaarufu ‘Mzee wa Mapangoni. Lugina na familia yake wamekuwa wakiishi kwenye pango hili linalokadiriwa kuwa na urefu wa zaidi ya mita 15.
Pango hili linalopatikana kijiji cha Igange, Manispaa ya Tabora, lina vyumba vinne na sebule. Lugina hutumia umeme wa nishati ya jua kutazama luninga na kupata mwanga.
Baba wa familia hiyo anasema hahofii kuwepo kwa wadudu kama nyoka na wengine kwa sababu si wadudu wakali, labda wakichokozwa ndipo hushambulia binadamu.
Comments are closed.