Lucy Komba Afunguka “Mtoto Wangu Wa Kwanza Nimezaa Na Mbasha” – Video
Staa wa kitambo kwenye anga la Bongo Muvi, Lucy Komba amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa mtoto wake wa kwanza aliyemzalia nchini Tanzania, alizaa na mwimbaji wa nyimbo za Injili na mfanyabiashara, Emmanuel Mbasha.
Akizungumza na Global TV katika mahojiano maalum, Lucy amesema watu wengi walikuwa wakijiuliza mambo kibao kuhusu maisha yake na msanii anayecheza naye kwenye Tamthiliya ya Malaika, ajulikanaye kwa jina la Ibra.