The House of Favourite Newspapers

 Exclusive! Mama Dangote: Mimba Ingeniua

0

KWA miezi kadhaa kumekuwa na minong’ono mingi mno kuhusiana na mama mzazi wa mwanamuziki mkubwa wa Afro-Pop barani Afrika kutoka nchini Tanzania, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aitwaye Sanura Kassim almaarufu Mama Dangote, kuwa ana mimba, lakini mwenyewe amefunguka kila kitu, IJUMAA lina exclusive story.

 

Katika mahojiano maalum (exclusive interview), Mama Dangote au Bi Sandra, anasema kuwa, kama angethubutu kubeba ujauzito, basi mimba hiyo ingeweza kumuua kutokana na umri wake.

 

SINTOFAHAMU

Taarifa za mimba ya Mama Dangote ambaye ni mke halali wa Maisara Shamte almaarufu Uncle Shamte, ziliibua sintofahamu kutoka kwa wataalam mbalimbali wa kiafya ambao waligawanyika makundi matatu; kuna waliosema inawezekana, kuna waliosema haiwezekani kutokana na umri wa mama huyo kuvuka miaka 50 na kuna waliosema ‘ya Mungu mengi’ wakimaanisha hakuna linaloshindikana chini ya jua.

 

Lakini kuna walioshangazwa na habari hizo na kusema Mama Dangote abebe mimba sasa hivi kwa sababu gani?

 

ANA KWA ANA NA IJUMAA

Hata hivyo, kwa mara ya kwanza, Mama Dangote au Kubwa la Maadui kama anavyopenda kujiita, amezungumza mambo mengi ya ana kwa ana Gazeti la IJUMAA alipokuwa dukani kwa mtoto wake wa kike, Esma Khan almaarufu Esma Platnumz lililopo Afrika Sana jijini Dar, mapema wiki hii;

 

IJUMAA: Habari za siku tele Mama Dangote? Vipi hali yako unaendeleaje?

MAMA DANGOTE: Habari yangu Alhamdulillah naendelea vizuri. Haya una mpya gani maana hapo najua una jambo?

 

IJUMAA: Hapana, ni kawaida tu, kwanza hongereni sana kwa duka zuri la vitambaa.

MAMA DANGOTE: Asante sana, pongezi zote ziende kwa Esma maana yeye ndiye mwenye duka, lakini tunamshukuru Allah mambo yanasogea sawia.

 

IJUMAA: Ila Mama Dangote unazidi kuwa kijana kila siku zinaposogea, nini siri yako?

MAMA DANGOTE: Naachaje sasa kuwa kijana kwa sababu mimi si ndiye mama lao? Sina mawazo yoyote, nakula vizuri, nalala vizuri, kiukweli sina matatizo yoyote yale unavyoniona hapa, sasa kwa nini nizeeke?

 

IJUMAA: Inaonekana mama unajivunia sana mtoto wako Diamond au Simba…

MAMA DANGOTE: Jamani ni mama gani ambaye asingejivunia kuwa na mtoto kama Diamond? Cha muhimu sana ninamuomba Mwenyezi Mungu azidi kumpa maarifa siku hadi siku. Hiyo ndiyo dua yangu ya kila siku.

 

IJUMAA: Watu wanakuchukulia tofauti, wanajua unaringa kutokana na ustaa alionao Daimond, hii imekaaje?

MAMA DANGOTE: Si kweli kabisa, kwanza mimi siringi, ninaringia nini sasa? Maana ustaa ni wa mtoto, inakuwaje ninaringa mimi? Mimi ninajivunia tu nimezaa mtoto ambaye amekuwa nyota karibu dunia nzima, ni hivyo tu.

IJUMAA: Vipi kuhusu hii ishu ya ujauzito mama maana imesemwa sana, je, ni kweli wewe ni mjamzito?

 

MAMA DANGOTE: Wewe hapa ukiniangalia mimba imekalia wapi hapa? Halafu nibebe mimba sasa hivi ninatafuta nini mimi? Maana hiki ni kipindi cha mimi kurudi ujana; yaani nikae tena ninanyonyesha? Ningebeba mimba na umri huu si ingeniua? Kama Shamte anataka mtoto anaye wa kusingiziwa yule mdogo.

 

IJUMAA: Kwani ni mtoto wa kusingiziwa?

MAMA DANGOTE: Ndiyo; mwenyewe si alimkana kabisa kwenye redio hukuona eeh; yaani nina wajukuu nikazae tena? Hao wananipakazia tu, mimi sina mpango huo.

 

IJUMAA: Mama Dangote kuna habari kuwa wewe ndiye msemaji wa mwisho wa mwisho (last say) kwa mwanao Diamond, ukisema kitu umesema, hilo vipi mama lina ukweli kiasi gani?

 

MAMA DANGOTE: Sasa kama Diamond hatanisikiliza mimi, atamsikiliza nani? Na ndiyo maana watu wanasema hivyo na Diamond anabarikiwa kila siku kwa sababu ananiheshimu sana na kunisikiliza mimi mama yake mzazi.

 

IJUMAA: Vipi akina Tiffah na Nillan walioko Sauzi kwa mama yao Zari watarudi lini tena Bongo?

MAMA DANGOTE: Watarudi tu maana huku si ndipo nyumbani kwao?

IJUMAA: Asante mama kwa ushirikiano wako.

 

MAMA DANGOTE: Asante sana, karibu tena Inshallah!

Hivi karibuni Mama Dangote amekuwa akitrendi kwa madai hayo kwamba ameamua kumtafutia Diamond au Mondi mdogo wake, lakini sasa ni rasmi kwamba mjadala huo umefungwa kutokana na mahojiano haya maalum na Gazeti la IJUMAA.

 

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply