Fundi Rangi Aliyejibiwa ‘SMS’ Na Rais Samia Akimuomba Simu Akiwa China Afunguka- Video
Fundi rangi anayejulikana kwa jina la Pascal amefunguka kupitia Global TV mara baada ya Maoni yake kujibiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan hapo jana Septemba 4, 2024.
Pascal ameeleza kuwa kazi ya Upakaji wa rangi katika majumba ameinza tangu mwaka 2013 na wapo pia baadhi ya wanawake wanaifanya kazi hiyo.
Ikumbukwe Pascal alijibiwa maoni yake na Rais Samia kuwa ombi lake litafanyiwa kazi hii ni mara baada ya kumuomba Simu ya mkononi kwa ajili ya kuendelea kutangaza vyema shughuli anayofanya kwa kuirekodi vizuri.