
Lakini mwisho ilionekana suala hilo lilishindikana na mwisho usiku huu, Caf imetangaza rasmi kuwa Serengeti Boys au Tanzania ndiyo iliyofuzu michuano hiyo ya vijana Afrika.
Katika mechi ya mwisho, Serengeti Boys ilifungwa bao 1-0 ikiwa ni baada ya kushinda 3-2 nyumbani Dar es Salaam na mfungaji wa bao la Congo nyumbani kwao akiwa ni kijeba huyo aliyekuwa amekomaa sura ile mbaya lakini akachezea timu ya watoto.


Comments are closed.