#Exclusive Video: Designer Mkongwe Jadore Aahidi Kutoa Sare Za Shule Kwa Wanafunzi 5,000
Mwanamitindo maarufu hapa nchini na nje ya nchi, Jadore Couture @j_adorecouturetz amesema kuwa hakuna kitu kilichokuwa kinamuumiza akiwa mdogo kama kwenda shule bila viatu ndiyo maana ameamua kufanya maonyesho ya mavazi kwa ajili ya harambee ya kukusanya fedha, ili kununua sare za shule na vifaa vingine kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Akifanyiwa mahojiano na Global TV, Jadore alisema atafanya harambee hiyo Desemba 16, mwaka huu katika Hoteli ya Serena, ambapo wanatarajia kuwafikia wanafunzi 5,000 ambapo atakuwa anaifanya kila mwisho wa mwaka kwani Januari, watoto ndiyo wanaenda shule na wengine wanakuwa hawana sare za shule wala viatu.