The House of Favourite Newspapers

EXCLUSIVE YA YA ALIKIBA ATAKACHOFANYA KABLA YA KUFUNGA MWAKA

STAA wa Bongo Fleva, Ally Salehe Kiba a.k.a Alikiba ameweka wazi kuwa Desemba 29, 2018 ataachia nyimbo zake mbili na kuzindua kinywaji chake cha Mofaya Energy Drink.

 

Kiba amesema ngoma hizo ataziachia kwenye shoo yake kubwa ya kufunga mwaka na muimbaji maarufu Afrika, Yvonne Chaka Chaka kutokea Afrika Kusini ikihairishwa hadi February, 2019.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kiba ameandika;

“BREAKING & EXCLUSIVE NEWS!!!! Kuelekea kwenye show yangu kubwa ya mwaka #FungaMwakaNaKingKiba tarehe 29 December pale @nextdoor_arena – nitaachia “HITS” zangu mbili kabla mwaka haujaisha pamoja na kuizindua rasmi kinywaji changu cha #MofayaEnergyDrink.

Sema kuna mabadiliko ya tarehe ya show yangu na Mama Yvonne Chaka Chaka pamoja na King Of Best Melodies @bellachristian – kutoka December to February 2019, the month of Love ❤ :
Lakini sasa… siku hiyo ya tarehe 22 December 2018 si ndio FIESTA finale , so I’ll be performing katika Finale ya Msimu wa come back ya Fiesta na wanangu kutoka @kingsmusicrecords :
Na kumalizia mwaka basi tukutane Mombasa on New Year Eve tarehe 31 December —cheers to the New Year Mombasani 🇰🇪!”

 

 

Kwa sasa Alikiba anafanya vizuri na wimbo unaokwenda kwa jina la Mwambie Sina alioshirikiana na kundi lake la Kings Music ambalo pia kwa sasa linafanya vizuri na wimbo uitwao, Toto.

BREAKING: Rais Magufuli Akihutubia wakati Akitia Saini Mradi wa Stiglers Gorge

Comments are closed.