The House of Favourite Newspapers

EXCLUSIVE: LULU Azua Mjadala Uraiani – Video

NI baada ya kubadilishiwa kifungo na kupewa kifungo cha nje ambapo ameachiwa na kutoka gerezani Jumamosi Mei 12. Mambo mengi yamesemwa lakini sheria ni msumeno na haina budi kuheshiwa.

Lulu ametoka kimya kimya na taarifa zake zilianza kusikika Jumapili usiku na Jumatatu kuthibitishwa na mamlaka husika ambayo ni magereza.

Minong’ong’o ya kuachiwa kwa Lulu imeibuka katika mitandao, uraiani na sehemu mbalimbali huku baadhi yao wakidai imekuwa mapema sana kuachiwa ikilinganishwa na kosa alilohukumiwa na nalo la Kumuua Kanumba bila kukusudia, wengine wakidai adhabu imekuwa fupi, na wengine wakisema ni haki yake kuachiwa kwa mujibu wa sheria.

Wasikie wadau wanasemaje na sheria inasemaje.

Mama Kanumba Afunguka Lulu Kuachiwa

Comments are closed.