The House of Favourite Newspapers

Exim Bima Festival 2024: Burudani Yenye Lengo la Kuboresha Huduma za Afya ya Akili

0

Mwezi Septemba, Benki ya Exim Tanzania inawakaribisha Watanzania wote na wadau mbalimbali kujumuika pamoja kwa ajili ya jambo muhimu na la kipekee; Afya ya Akili.

Ikiwa inasherehekea miaka 27 ya kuwahudumia Watanzania tangu kuanzishwa kwake, benki ya Exim inakuja na Exim Bima Festival 2024, ikiwa na kaulimbiu ‘Amsha Matumaini’, ambayo itafanyika mnamo tarehe 28 Septemba 2024 katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Hili ni zaidi ya tamasha, ni wito kwa kila Mtanzania kuchukua hatua kuongeza uelewa na msaada kwa watu wenye tatizo la afya ya akili.

Wakati changamoto za afya ya akili zikiongezeka nchini, tamasha hili ni fursa ya kipee kwa watu binafsi, wadau, taasisi, na sekta mbambali kuungana katika kukusanya fedha kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wale wanaoathirika na tatizo la afya ya akili.

Exim Bima Festival 2024 ni moja ya malengo ya mpango wa ‘Exim Cares’ wa Exim Bank Tanzania. Tamasha la mwaka huu limepanga kuelekeza nguvu zake katika kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa wa bima katika jamii yetu huku likijikita katika kusaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za afya ya akili na ustawi wa jamii ya Watanzania kote nchini.

Benki ya Exim imejiwekea lengo la kukusanya jumla ya TZS milioni 300 ndani ya miaka mitatu ijayo ili kugharamia huduma muhimu na maboresho ya miundombinu katika vituo vya afya ya akili.

“Tatizo la afya ya akili sio tu ugonjwa, ni suala la kijamii zaidi. Wanaoathirika ni familia zetu, marafiki zetu, mfanyakazi mwenzako, na jamii zetu. Kwa pamoja, tunaweza kubadirisha hadithi hii. EXIM BIMA FESTIVAL 2024 sio tu kwa ajili ya kujumuika na kufurahia pamoja; pia tunalenga kuongeza uelewa na kubadilisha maisha ya Watanzania,” anasema Stanley Kafu, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania.

Kafu anaongeza, “Tunapojumuika pamoja, tunavunja ukimya, tunaondoa unyanyapaa, na kujenga jamii ambayo inalipa suala la afya ya akili kipaumbele na kuhakikisha waathirika wanapata huduma bora wakati zinapohitajika. Karibu tuungane Kuamsha Matumaini Yao.”

Tamasha hili linaahidi burudani mbalimbali za kusisimua kwa kwa watu wazima na watoto, kuhakikisha inakuwa siku iliyojaa furaha, michezo, na mashindani ya kuvutia. Washiriki watapata fursa ya kushiriki katika michezo na kupata burudani, huku wakiungana kugusa na kubadlisha maisha ya Watanzania wengi popote walipo nchini.

Kwa nini ujali? Kwa sababu afya ya akili inatuathiri sote. Wizara ya Afya imeripoti ongezeko la kutisha la asilimia 82 la visa vya afya ya akili katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Kutoka visa 386,358 mwaka 2012 hadi 2,102,726 mwaka 2021 na hivyo kufanya mahitaji ya huduma za afya ya akili kuwa makubwa zaidi nchini.

Kwa bahati mbaya, uwezo wa Tanzania kukabiliana na changamoto hii unakwamishwa na uhaba wa wataalamu wa afya ya akili, miundombinu, vifaa vya matibabu, na dawa.

Katika jumla ya mikoa 28 nchini, mikoa mitano tu ndiyo ina vituo vinavyotoa huduma za afya ya akili zinazokidhi viwango. Ukubwa na hatari ya tatizo hili ni takwimu kuonesha kuwa kundi lililoathirika zaidi ni la wenye umri wa kati ya miaka 15 na 39 ambao ndio nguvu kazi ta taifa na hivyo kuhitajika juhudi za ziada kuokoa kizazi hiki kwa ajili ya ustawi na maendeleo ta Tanzania.

Jitihada hizi za Exim Bank zinaendana na malengo makubwa ya Serikali ya kuhakikisha kila Mtanzania anafikia na kupata huduma bora za afya wakiwemo wagonjwa wa afya ya akili. Kwa kuboresha huduma za afya ya akili, benki inalenga kuchangia katika ujenzi wa mtandao wa jamii ambayo inaweza kufikia huduma kwa haraka, gharama nafuu, wakati wowote na mahali popote Tanzania.

Naye akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja wa Idara ya Bima wa benki hiyo, Tike Mwakyoma alisema, ”Tunatambua na kuheshimu mchango wa wadau wetu kutoka kampuni za bima ambao tumekuwa pamoja tangu tamasha lililopita mpaka kufanikisha la mwaka huu. Tuendelee na umoja huu kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote na taifa kwa ujumla.”

“Benki ya Exim tunakukaribisha wewe, rafiki yako, mdau yeyote au taasisi ambao wanaguswa na changamoto hii na wangependa kuchangia juhudi hizi kufanya hivyo kupitia akaunti maalumu yenye Jina: Exim Cares na Akaunti Na: 0010060253 au tembelea tovuti ya benki yetu kwa maelezo zaidi, www.eximbank.co.tz.

Karibu tuifanye Exim Bima Festival 2024 iwe zaidi ya burudani. Jiunge nasi Tuamshe Matumaini ya Watanzania Wenzetu,” anahitimisha Bi. Kauthar D’souza, Meneja Mkuu kutoka Idara ya Masoko na Mawasiliano katika benki ya Exim Tanzania.

Leave A Reply