The House of Favourite Newspapers

Exim Yatangaza Likizo Ya Malipo Ya Mikopo Ya Bilioni 160

0

Benkiya Exim imetangaza msamaha wa likizo ya malipo ya mikopo kwa wateja wakewakubwa, wa kati na wadogo walipo katika sekta zilizo athirika zaidi kiuchumikutokana na athari za mlipuko wa ugonjwa wa virus vya Corona (COVID 19). Hatuahiyo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na benki hiyo katika kuwasaidiakifedha wateja wake waliopo sekta ambazo zimeathiriwa zaidi na athari zamlipuko wa ugonjwa huo.

 

Kwa mujibuwa taarifa iliyotolewa hii leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, BwJaffari Matundu  alisema msamaha huowenye thamani ya zaidi ya sh Bilioni 160 umeanza mwezi Juni mwaka huu, ukihusishalikizo ya malipo ya mikopo kwa wateja na nyongeza ya muda wa urejeshaji wamikopo  ili kusaidia wateja wa benki hiyokatika sekta mbali mbali kutokana na athari za janga hilo kwenye biashara zao.

 

“Benkiinaelewa mahitaji ya wateja wetu wakati huu na tunafanya yote yanayowezekanakuwasaidia ili waweze kuvuka salama katika kipindi hiki kigumu. Jitihada hizihaziishii tu kwenye misamaha hii tunayoitoa bali pia kupitia huduma za ushaurikuhusu mikakati ya biashara ili kuhakikisha kwamba  biashara za wateja wetu zinadumu nazinafanyika kwa mafanikio zaidi,” alisema.

 

Kwa mujibuwa Bw Matundu msamaha huo unazingatia vigezo mbalimbali kwa kila mteja kwa kuwaathari za COVID-19 hazikuwa sawa katika sekta zote. “Tunafarijika kwa kuwatayari wateja waliopo kwenye sekta zilizoathiriwa zaidi wameshaanza kusaidiwa. Mazungumzona wateja wengine bado yanaendelea ili kutambua hatua mbali mbali zinazofaa kulinganana aina ya biashara, ” aliongeza.

“Sikuzote Benki ya Exim, tunaamini katika kufanya kazi kwa bidii leo kwa ajili yakesho bora kwa wateja wetu, biashara zao na jamii kwa jumla, ni kwa mtazamohuo  tumepitisha hatua kama hii katika wakatihuu mgumu.Tunaendelea kujitolea kushughulikia mambo haya na kupata suluhishosambamba na mamlaka pamoja na  Serikali katikakuhakikisha uchumi wetu unaendelea kuwa thabiti wakati wa nyakati hizi ngumu.” alihitimisha.

Leave A Reply