The House of Favourite Newspapers

Fabregas Aanza Mambo Monaco

Cesc Fabregas

MONACO inaelekea imelamba dume kwa kitendo chao cha kumsajili kiungo mkongwe, Cesc Fabregas. Fabregas alionyesha cheche zake kwenye mechi yake ya kwanza Monaco wakati ilipofungana bao 1-1 na Marseille, wikiendi iliyopita.

 

Pamoja na kuwa Fabregas hakufunga kwenye mchezo huo wa Ligue 1, lakini alipandisha morali ya wenzake katika timu kutokana na jinsi alivyokuwa anachezesha timu. Kiungo huyo wa Kihispania alionyesha soka la kiwango cha juu na pasi za uhakika.

Pia muda mwingi wa mechi akiwahamasisha wenzake kujituma kwenye mechi hiyo ya ugenini. Kutokana na jinsi alivyoonyesha umahiri wake kwenye mchezo ule ni wazi ana nafasi kubwa ya kuisaidia Monaco, ambayo ipo kwenye nafasi za mkiani kwenye Ligue 1.

Comments are closed.