visa

Facebook Yaanzisha Programu Kulinda Kuingiliwa Data Zako

MTANDAO wa FACEBOOK umeanzisha mfumo wa kufichua data inazozikusanya kutoka kwa watumiaji wake.   Wengi hawapendi wanachokiona. Programu iliyowekwa na mtandao huo inayoitwa Off-Facebook Activity, yaani nje ya shughuli za Facebook, itaonyesha programu zote na mitandao inayotuma taarifa kukuhusu wewe mteja kwenye Facebook, ambazo hatimaye hutumiwa kulenga matangazo kwa ubora zaidi.

Programu hiyo mpya itakuwezesha kuwa na uwezo wa kufuta historia yako na kuzuia tabia ya mtandao huo kuingiliwa tena.  Lakini mtaalamu mmoja anasema hatua hiyo huenda isiwe na athari kubwa katika faida ya kampuni ya Facebook.

Kwa sasa, mpango huo unaendelea taratibu huku Ireland, Korea Kusini na Hispania, lakini lengo ni hatimaye kutoa huduma hii kote duniani.  Utoaji wa huduma hii unakuja wakati Apple na Mozilla tayari wamekwishachukua hatua za kuizuia Facebook na huduma nyingine za mtandao kuwachunguza watumiaji kupitia mtandao mmoja hadi mwingine kwa njia ya kurambaza.

Programu hii itawawezesha watumiaji kutambua ni watu gani wengine au programu zipi zinazotumia data zako katika facebook

Zaidi ya hayo, wasimamizi wa ushindani nchini Ujerumani walikuwa wameiambia Facebook kuwa inapaswa kuweka ukomo wa namna ilivyokusanya na kujumuisha data zake juu ya ya watumiaji wa mtandao wake la sivyo itatakiwa kujibu juu ya hofu za watumiaji kuliko ilivyofanya awali.

Facebook hukusanya data zaidi ya zile zilizopo kwenye ukurasa wako kwa sababu labda umeamua kutumia mtandao wa kijamii kuingia katika Facebook au kutoingia katika programu(app), au hata kuna uwezekano mkubwa wa kuchukua data zako kwa sababu mtandao hutumia kitu kinachoitwa Facebook Pixel kufuatilia shughuli zako mtandaoni.

Hii ndiyo sababu unaporamabaza mtandao pengine ukitaka kununua bidhaa kama viatu , utabaini kuwa kuna tangazo la kibiashara linachungulia ghafla kwenye ukurasa wako wa Facebook na baadaye utaona ujumbe pengine kama baada ya nusu saa hivi ukipendekeza viatu unavyoweza kuvinunua ambavyo umekuwa ukivisaka kwenye mtandao wako wa Dacebook

Kuanzishwa kwa programu ya Off-Facebook Activity kutakusaidia kufichua kikamilifu ni data gani au kurasa gani za mtandao zinashirikisha taarifa kuhusu wewe.  Facebook inasema simu ya kawaida ya smartphone ina programu 80 na 40, kati hizo hutumiwa na huenda zinaweza kuwa zaidi.

Utaweza sasa kukata mawasiliano ya data zako na utambulisho wako wa Facebook – ama kwa kampuni au kwa vyanzo binafsi vinavyokusaka. Ikiwa utatumia fursa hii, itamaanisha kuwa yale matangazo ya viatu yataacha kujitokeza katika simu yako wakati wote.

Ni muhimu kusisitiza kwamba Facebook bado itakuwa inakusanya data, lakini kutakuwa hakuna utambulisho – wanaweza kujua kuwa watu wengi wamekuwa wakitafuta bidhaa fulani, lakini hawatajua kuwa wewe ulikuwa miongoni mwao.

Off-Facebook Activity imekuwepo zaidi ya mwaka mmoja na utekelezaji wake unatokana na ahadi aliyoitoa Mark Zuckerberg katika kikao cha mwaka jana ambapo aliahidi kuwapatia watumiaji wa mtandao wa Facebook udhibiti mkubwa wa namna taarifa (data) zao zinavyotumiwa.
Toa comment