Aidha Said amewashukuru wachezaji wote waliojitokeza katika mashindano hayo na kuwapongeza wale wote walioshinda na ambao hawakufanikiwa kushinda akiwahimiza kuendelea kucheza mchezo huo na kujitokeza katika mashindano yajayo.
Kwa upande wake Mchezaji wa gofu wa kulipwa, Mollel amesema namshukuru Mungu kwa kumuweza kupata ushindi licha ya kiwanja cha Dar Gymkhana kuwa kigumu kidogo.
Amesema michuano ilikuwa mikali hata hivyo amefanikiwa kupata ushindi na kwamba anaishukuru familia ya Nkya kwa kuamua kuleta mashindano hayo ambayo yamewaleta pamoja Wachezaji wa gofu nchini.
”Familia hii imefanya kazi kubwa kuhakikisha kuna kuwepo na mashindano haya, hakika tumemuenzi kweli Lina Nkya,” amesema Mollel
Naye Fadhili Nkya amesema mishuano hiyo ilikuwa migumu lakini anamshukuru Mungu kwa kumuweza kuibuka kuwa mshindi na hatimaye kuiwakilisha Tanzania nchini Dubai.
Michuano ya gofu ya Lina PG Tour imeandaliwa na familia ya Said Nkya kwa kushirikiana na Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU) kwa lengo la kumuenzi marehemu Lina.
Wachezaji wawili wa kulipwa wa gofu wanatarajiwa kwenda nchini Dubai Falme za Kiarabu kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya mchezo wa gofu utakaofanyika mwakani.
Wachezaji hao ambao ni Fadhil Nkya kutoka klabu ya Gymkhana Dar es Salaam na Nuru Mollel kutoka klabu ya Arusha Gymkhana wamepata fursa hiyo baada ya kushinda katika mashindano ya Lina PG Tour ambayo yamefanyika kwa lengo la kumuenzi mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Gofu marehemu Lina Nkya.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa fainali ya mashindano hayo katika viwanja vya Dar Gymkhana, Mratibu wa Lina PG Tour, Said Nkya amesema mashindano yalikuwa mazuri na kwa sasa wameweza kuwahamasisha watanzania hasa wafanyabiashara ambao wameshaanza kudhamini michuano hiyo.
”Tumepata ushirikiano mkubwa katika vilabu, mashindano yalikuwa mazuri na tayari tumewahamasisha watanzania hasa wafanyabiashara na tumeanza kupata wadhamini kutoka hapa nchini,” amesema Nkya ambaye ni mume wa marehemu Lina