Fahamu kinachosababisha kiharusi (Brain Stroke)

UKISEMA mtu fulani ana ugonjwa wa kiharusi maana yake viungo vyake vimepata ganzi au kitaalam huitwa stroke na kusababisha mwili kutojiweza au kwa maneno mengine ni kuwa mtu huyo hulemaa katika kile kiungo kilichokumbwa na ugonjwa huo.  Dalili za mtu kuugua kiharuhsi hutokea na kutoweka ghafla. KINACHOSABABISHA KIHARUSI Watu wengi wangependa kujua kinachosababisha mtu kupatwa na kiharusi. Kinachosababisha ni pale eneo fulani la ubongo linapokosa damu kwa saa 24 au zaidi na ndiyo maana Wazungu wakauita ugonjwa huu brain attack.

Mtu pia anaweza kupatwa na kiharusi kama itatokea kuna kizuizi kwenye mwili wake kinachofanya damu isisafiri kwenye mishipa yake hivyo kusababisha kupasuka baadhi ya nyama muhimu kwenye ubongo ambazo kitaalam huitwa vital brain tissue. Hali hii ikitokea inakuwa haina tofauti sana na inapotokea mishipa ya arteri katika mwili hupasuka na mtu huyo kukumbwa ghafla na ugonjwa wa moyo ambao kitaalam huitwa heart attack.

KIHARUSI CHA HAEMORRHAGE

Mtu hukumbwa na kiharusi hiki kiitwacho kitaalam haemorrage baada ya kupasuka mshipa kwenye ubongo na kusababisha damu kuvuja, yaani haemorrhage. Hali hii inapotekea ni kwamba damu iliyovuja hukandamiza ubongo, hali inayosababisha uharibifu mkubwa kwenye ubongo kwa kuwa ubongo ni kiungo laini sana katika mwili kisichotaka kuguswa na kitu kingine.

Kitendo cha damu hiyo kuganda katika ubongo licha ya kuharibu eneo hilo laini la ubongo katika fuvu la kichwa, husababisha uharibifu wa chembe hai kwenye ubongo. Hivyo hali hiyo huhatarisha maisha ya mgonjwa na huitwa kitaalam cerebral haemorrhage ambapo uvujaji wa damu hufanyikia ndani ya ubongo, jambo ambalo ni la hatari kwa maisha ya mgopnjwa.

Mtu pia anaweza kukumbwa na kiharusi baada ya kupasuka mshipa wa damu ambao unazunguka ubongo na hali hiyo inapotokea huitwa kitaalam kuwa ni sabarachindid. Hali hiyo pia ni hatari kwa maisha ya mtu aliyepatwa na tatizo hilo.

KIHARUSI INSCHAEMIA

Kuna kiharusi kiitwacho Ischaemia. Aina hii ya kiharusi hutokea kutokana na mshipa uitwao kitaalam arteri unapoganda damu. Hali hiyo ikitokea damu hushindwa kusafiri hadi kwenye ubongo, hivyo mtu kukumbwa na kiharusi kiitwacho Ischaemia, neno ambalo kwa Kigiriki maana yake ni kuzuia damu.

Hali hiyo inaweza kutokea kwa kusababishwa na kitu kinachoitwa thrombosis ambapo damu huganda kwenye mshipa mkubwa wa arteri, mshipa huu ni muhimu sana katika mwili wa binadamu kwa kuwa ndiyo unaosafirisha damu kupeleka kwenye ubongo.

Hali hiyo inaweza pia kusababisha vimirija vidogovidogo vinavyopeleka damu kwenye ubongo kuziba na kitendo hicho wataalam wa afya au tiba huwa wanakiita lacunar stroke. Hata hivyo, aina hii ya kiharusi (lacunar stroke) wataalam wamegundua kuwa haina madhara makubwa sana kwa mtu ambaye amekumbwa nayo.

USHAURI NA TIBA

Kwa kawaida mtu akipatwa na kiharusi si rahisi kumtibu nyumbani, ni vema akawahishwa hospitalini ili akaonwe na daktari na kufanyiwa vipimo haraka.

Jambo la muhimu ikiwa mgonjwa ameanguka ni kuhakikisha kuwa kichwa chake kinainuliwa kidogo ili mate yake yasiweze kuingia kwenye njia ya hewa na kuziba hewa kwenda kwenye mapafu. Akiwahishwa hospitalini daktari akimuona ataweza kumsaidia kwa kumpima na kumpa dawa husika.


Loading...

Toa comment