The House of Favourite Newspapers

Fahamu Kuhusu Mashindano Mapya Barani Afrika ya CAF Super League

0
Rais wa FIFA Gianni Infantino akiwa na Rais wa CAF Patrice Motsepe

RAISI wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika, Patrice Motsepe ametangaza kuanzishwa kwa mashindano mapya ya vilabu Afrika yatakayo julikana kama “CAF Super League” alipokuwa akizungumza katika mkutano mkuu wa CAF uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha nchini Tanzania.

 

 

Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi Agosti,2023 ikihusisha timu 24. Malengo makubwa ya michuano hiyo ni kusaidia timu za Afrika kiuchumi ili kuweza kuendana na kasi ya ukuaji wa mchezo wa mpira wa miguu na kuweza kushindana na timu kubwa nje ya Afrika.

 

 

Motsepe alisema “Ukiwa mchezaji wa mpira unakuwa na muda mchache wa kufanya kazi kwahiyo inabidi upate pesa nyingi ili baada ya kustaafu mpira uweze kumudu kutunza familia, kwa Afrika timu hazilipi vizuri ukifananisha na ulaya ndo mana tunashindwa kuwabakisha wachezaji wetu wazuri” aliendelea kwa kusema “Kwa kutokuwa na wachezaji wazuri inapelekea ligi zetu kutotazamwa sana hii ikatufanya tuje na wazo la kuanzisha Africa Super League ili kuinua timu zetu kiuchumi na kupata wachezaji wazuri kukuza ligi zetu”.

 

    Kwa mujibu wa Motsepe, mashindano hayo yanatarajiwa kuongeza hamasa katika maendeleo ya soka barani Afrika

Bingwa wa michuano ya Africa Super League atapata kitita cha dola za kimarekani milioni 11.5 ambayo ni sawa na Zaidi ya billioni 27 za kitanzania, huku timu 24 zitakazo shiriki watapatiwa dola za kimarekani milioni 3.5 kila mmoja ambayo ni zaidi ya bilioni 8 za kitanzania kwa ajili ya usajili, malazi, chakula, usafiri na mengineyo.

 

Hawakuishia hapo pia kila nchi mwanachama wa CAF atapata dola za kimarekani milioni moja ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 2 za kitanzania kwa ajili ya kuendeleza na kukuza soka nchini mwao.

 

Picha ya pamoja ya baadhi ya wadau wa soka barani Afrika akiwemo Rais wa CAF Patrice Motsepe na Rais wa FIFA Gianni Infantino

Mashindano hayo yamepitishwa na Raisi wa FIFA, Giovani Vincenzo Infantino ambaye pia alikuwepo katika huo mkutano ambapo alisema “Nina furaha kuwepo nanyi leo siku ya leo, leo ni siku ya kipekee sana kwakuwa Afrika inapiga hatua kubwa katika mpira wa miguu , Super League ni kitu kikubwa sana kwa soka la Afrika na nitakuwa na furaha nikiweza kuhudhuria mechi za CAF Super League.”

Leave A Reply