The House of Favourite Newspapers

Fahamu Kwanini Infinix Note 10pro ni Bora Zaidi

0

Teknolojia imerahisisha kwa kiasi kikubwa swala la mawasiliano katika miaka mitano hii tumeona Makampuni mengi ya simu yakichuana vikali kupitia bidhaa zao moja ya kampuni inayoonekana kukimbiza kwasasa ni kampuni ya simu za mikononi Infinix.

Infinix tangu kutambulishwa Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 2018 imekuwa na ushindani mkubwa sana na makampuni mengine ya simu kama Samsung.

Infinix na Samsung wamejikuta katika ushindani mkubwa hasa kwenye simu hizi mbili Samsung A51 na Infinix NOTE 10pro.

 

Kamera

Infinix NOTE 10pro na Samsung A51 zina baadhi ya sifa za kufanana kama uwepo wa kamera 4 nyuma isipokuwa kamera kuu ya Infinix NOTE 10 pro ni ubora zaidi kulingana na namba ya pixel NOTE 10 pro ikiwa na MP64 na A51 ni MP48 na kwasababu hii tunasema Infinix imefaulu kwani Kamera ya nyuma ni kamera muhimu sana hasa ukizingatia Kamera ya NOTE 10 pro ina uwezo hadi wa kuscan document.

 

Processor

Kwa upande wa processor Infinix Note 10 Pro inatambulika kama simu bora sana kwaajili ya kucheza game kwani simu hii inakuja na processor ya MediaTek Helio G95na Samsung Galax A51 inakuja na Exynos 9611. Helio G95 ni pendwa sana kwa wapenzi wa games na Exynos 9611 kasi yake ipo kwenye matumizi ya application nyinginezo na si kwa games kwa hapa tunaweza sema kila simu imefaulu kwa aina yake kutokana na aina ya watu   wanaowalenga. Infinix inalenga zaidi vijana wenye kupenda kwenda na wakati na games ni moja ya starehe yao kubwa na Samsung ni kampuni yenye kulenga watu wa makamo basi hadi hapo kampuni zote mbili zimefaulu.

 

Ram

Kwa upande wa RAM ni wazi kuwa simu hizi zinalingana zote zikiwa na RAM ya GB 8, hapa lakini kwa upande wa Infinix Note 10 Pro unapata toleo lenye GB 8 za RAM huku kwa Galaxy A51 ukiwa unapata matoleo ya GB 4, 6 na 8

 

Uhifadhi wa Ndani (Rom)

Kwa upande wa uhifadhi wa ndani au ROM, Infinix Note 10 Pro inaongoza kabla hujabisha ngoja nikupe sababu Infinix Note 10 Pro inakuja uhifadhi wa GB 128 na 256 lakini mbali na hivyo sehemu ya kuweka memory card kwenye Infinix Note 10 Pro imejitenga na hivyo una uwezo wa kuweka laini mbili za simu pamoja na Memory card, Infinix Note 10 Pro ina uwezo wa kuchukua memory card ya Hadi TB 2 tofautina Galaxy A51 ambayo inaweza kuchukua Memory ya hadi TB 1 lakini pia Galaxy A51 haina nafasi ya kuweka memory ni lazima uchague uweke line moja ya simu na sim card ya pili uweke memory kadi na sikuweka line mbili za simu na memory card kwa wakati mmoja. Hapa tunasema NOTE 10pro imefaulu.

 

Sensor

Kwa upande wa Sensor au sensa simu zote zinakuja na sensa ambazo zinafanana ambazo ni Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass. Tofauti kubwa ambayo ipo kwenye Infinix Note 10 Pro ni pamoja na kuwa na sehemu ya Fingerprint pembeni kwenye sehemu ya kuwasha hii itakupa urahisi wa kufikia sehemu hii hata kwa mkono mmoja tofauti na Galaxy A51 ambayo inayo sehemu ya fingerprint kwenye kioo ambayo ni lazima kushika simu kwa mikono miwili.

 

Betri

Kwa upande wa betri simu ya Infinix Note 10Pro inaongoza kwenye upande wa betri kutokana na kuwa na betri kubwa ya 5000 mAh ambayo pia inaweza kujaa chaji kwa haraka kutokanana kuwa simu hii inakuja na teknolojia ya Fast charging ya hadi 33 Wh.

Tofauti na Galaxy A51 simu hii inakuja na betri ya 4000 mAh, ambayo inakuja na teknolojia ya fast charging yenye uwezo wa hadi 25Wh. Na hapa Infinix imefaulu.

 

Sifa Za Nje

Muundo

Tukianza na muundo simu ya Infinix Note 10 Pro ni simu bora kwenye kipengele hiki, hii inatokana na simu hii kuwa na muundo mkubwa kuliko Samsung Galax A51. Infinix NOTE 10pro ina urefu (height) inch 6.80, upana (width) inch 3.08, na kina (depth) inch 0.31.

Galaxy A51 ina inch 6.5 lakini ukiangalia kwenye swala la gharama Infinix NOTE 10 pro inapatikana kwa bei rafiki ukilinganisha na sifa zilizopo kwenye simu hiyo hapa tena Infinix amefaulu kwa asilimia kubwa.

 

Kioo

Tukija kwenye upande wa kioo, Infinix Note 10 Pro pia inaongoza kwenye kipengele hiki kwakuwa na kioo kikubwa zaidi, Infinix Note 10 Pro inakuja na kioo cha inch 6.95, tofauti na simu za Galaxy A51 yenyewe inakuja na inch 6.

Mbali na hayo Infinix Note 10 Pro inaongoza kwa resolution ikiwa na resolution ya hadi pixel 1080 kwa 2460, na Galaxy A51 ikiwa na resolution ya chini huku ikiwa inakuja na resolution ya pixel 1080 kwa 2400.

 

Upatikanaji

Kama umeelewa vizuri tofauti wa hizi simu mbili basi kwa upatikanaji wake tafadhali

tembelea duka lolote la simu karibu yako.

Leave A Reply