FAHAMU SARATANI YA MATITI NA JINSI YA KUJIPIMA

SARATANI ya matiti ni moja ya magonjwa yanayoongoza katika kusababisha vifo kwa kina mama duniani. Lakini licha ya ugonjwa huo kuwa tishio iwapo tutajizoeza kujipima sisi wenyewe mara kwa mara ili kuangalia iwapo tuna dalili za ugonjwa huo, suala hilo linaweza kusaidia kutambua uwepo wa ugonjwa huo mapema na kuanza matibabu haraka, hivyo kuepusha vifo. Kutokana na idadi kubwa ya vifo na kesi za kansa ya matiti duniani, utambuzi wa awali husaidia kupunguza vifo na mateso yanayotokana na ugonjwa huo kwa kiasi kikubwa. Pia utambuzi wa mapema wa ugonjwa huo hupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa na hata serikali husika.

Kwa mfano nchini Tanzania pekee, rekodi za hospitalini zinaonesha kuwa, kila mwaka wanawake 2,500 wa nchi hii wanaripotiwa katika hospitali kuu wakisumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya matiti.  Kati ya hao Na mtaalam wetu, A.Mandai2,500, wanawake 300 tuu ndio wanaoweza kuendelea na matibabu ya mionzi au upasuaji wa ugonjwa huu kupitia wataalamu wa ugonjwa huo nchini. Lakini wanaobakia ambao ni wengi huwa hawawezi kuendelea na tiba kutokana na kushindwa kugharamia tiba ya ugonjwa huo na sababu nyinginezo. Mara nyingi na kwa bahati mbaya  wagonjwa wengi mara wanapogundua

kujichunguza ili kufahamu kama ana ugonjwa huo au la. Ingawa watu wa umri wote wako katika hatari ya kupatwa na kansa ya matiti lakini ugonjwa huo unawapata zaidi wanawake baada ya umri wa miaka 40 na kuendelea. Lakini hii haimaanishi kwamba wanawake walio chini ya umri huo hawapaswi kujichunguza mara kwa mara kuhusu ugonjwa huo. Wasichana wawe na mazoea ya kujichunguza matiti yao toka wakiwa wadogo na kuangalia iwapo kuna mabadiliko yanayoweza kuashiria uwepo wa ugonjwa huo.

Pia wanawake wote wanashauriwa kujifanyia wenyewe uchunguzi wa kansa ya matiti kwa uchache mara moja kwa mwezi. Asilimia 40 ya kesi za ugonjwa wa kansa ya matiti hugunduliwa na wanawake kwa huhisi uvimbe, hivyo mazoea ya kujifanyia uchunguzi ili kuangalia kama wamepatwa na ugonjwa huo ni jambo muhimu sana. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kipimo cha mammography kinaweza kumsaidia mwanamke kugundua kansa kabla ya kufanya uvimbe, lakini kujichunguza mwenyewe kunamsaidia mwanamke

kuwajuza mapema wataalamu wa afya iwapo ataona mabadiliko yoyote yanayoweza kusababishwa na kansa ya matiti. Tunashauriwa kuwa, muda bora wa kujichunguza (breast self examination) ni siku 3 hadi 5 baada ya kuanza hedhi. Namna ya kujichunguza matiti au breast self exam ni kama ifuatavyo.

Kwanza kabisa ni vizuri zaidi uchunguzi huo ukifanywa wakati mtu akiwa amelala kwenye kitanda au akiwa mbele ya kioo kinachoweza kuonesha vizuri kiwiliwili hasa upande wa juu. Kama umesimama nyoosha mkono wako na kuukunja hadi kiganja cha mkono wa upande unaotaka kupima kiwe nyuma ya kisogo. Kwa kutumia kiganja cha mkono mwingine papasa na kubonyeza sehemu zote za titi kwa mduara, tokea pembeni huku ukibonyeza taratibu kuelekea kwenye chuchu hadi  karibu na ndani ya kwapa.

Baada ya hapo papasa na kubonyesha ziwa upande wa chini. Angalia iwapo utahisi tezi au uvimbe wowote, ngozi kuwa ngumu au mabadiliko ya aina yoyote. Kama umelala nyoosha mkono na kuulaza ili nao ulale kwenye kitanda pia. Baada ya hapo papasa na kubonyeza taratibu titi upande wa juu halafu papasa au bonyeza titi kwa pembeni karibu na ndani ya kwapa. Baada ya hapo papasa na kubonyesa titi upande wa chini na chuchu pia. Itaendelea wiki ijayo

kwamba wana kansa ya matiti huwa tayari ugonjwa huo hatari umeshasambaa katika mwili na mishipa ya limfu, hivyo wataalamu wa tiba huwa na muda mchache wa kumsaidia mgonjwa, na mara  nyingine pia baada ya kipindi kifupi  mgonjwa huwa katika steji za mwisho za ugonjwa huo. Yote hayo yanaonesha umuhimu wa kila mwanamke kufahamu namna ya

Loading...

Toa comment