MAPAFU ndio kiungo kinacho-tegemewa sana katika mwili kama utafanya mazingatio maana ubongo ukikosa oksijeni ndani ya dakika 5 kwenda juu seli za ubongo hupata athari na hufa. Mapafu yanahusika katika uchukuaji wa oksijeni inayotoka puani au mdomoni na kuipeleka katika sehemu husika mwisho hufika katika vifuko vidogo sana (alveoli), vipo milioni 300 na zaidi ambapo oksijeni hutoka kwenye kuta hizo na kuingia katika damu na kusambazwa sehemu zote za mwili kupitia moyo.
Tatizo la mapafu kujaa maji hutokea pale ambapo kunakuwa na mkusanyiko wa maji kati ya kuta mbili zinazozunguka mapafu. Kujaa huku kwa maji husababisha mgonjwa kupata shida ya kupumua vizuri. Sababu za mapafu kujaa maji zinaweza kuelezewa kutokana na aina ya maji yaliyojaa: Kwa mfano kuna kitu kinatajwa kuwa ni Transudate – hapa maji hutoka kutoka kwenye mishipa ya damu na kuingia kwenye mapafu hasa kwa watu ambao wana magonjwa yafuatayo: Moyo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kitaalamu huitwa congestive cardiac failure, ini kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kitaalamu tunasema liver failure na figo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi yaani renal failure.
Lakini pia wenye Exudate – hapa maji hujaa kutokana na kuta zinazozunguka mapafu kuwa na maji kitaalamu pleura husababisha mapafu kuvimba. Mtu anaweza mapafu yake kujaa kutokana na magonjwa ya mapafu mfano: Kansa ya mapafu au ya titi, ugonjwa unaoitwa Lymphoma, Kifua kikuu (TB), vichomi, figo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi au kuwa na majipu ndani ya tumbo.
DALILI YA UGONJWA
Mtu ambaye amepatwa na tatizo la mapafu kujaa maji huwa na dalili za kusindwa kuhema vizuri, kusikia maumivu ya kifua au hukumbwa na Kifua Kikuu ambapo jasho jingi kutoka kipindi cha usiku, hukohoa damu, na hupungua uzito kwa kasi ya kutisha. Dalili nyingine ni mgonjwa kuwa na vichomi, pia hupatwa na homa, hukohoa makohozi yenye rangirangi, inaweza kuwa damudamu au manjano.
UCHUNGUZI NA VIPIMO
Mtu ambaye ana tatizo la mapafu yake kujaa maji anatakiwa kufanyiwa kipimo cha kuchukuliwa picha ya kifua kikuu, kwa kutumia x-ray, au kupimwa kwa Ultrasound ya kifua ama CT-scan au Thoracentesis na wakati mwingine hutumika vipimo vya damu. Itategemea daktari ataamuaje ili kubaini tatizo.
MATIBABU
Kwa sababu ya kusababisha matatizo ya kupumua inabidi kuanza na ABC za kuokoa maisha, angalia mfumo wa hewa na kadhalika. Daktari anatakiwa kutibu magonjwa yanayosababisha kupunguza maji kwenye mapafu kwani kunaweza kutumika kwa ajili ya kipimo au matibabu ya kumpa nafuu mgonjwa. Kila mtu aonapo dalili tulizozitaja anatakiwa kwenda kupimwa na daktari.
Comments are closed.