The House of Favourite Newspapers

Fahamu tatizo la mzio au allergy-2 Dalili za mzio (allegy)

0

3-main-types-of-allergy
Wiki iliyopita tulieleza matatizo ya mzio na watu wanapataje lakini hatukueleza dalili zake.

Leo tunaeleza dalili za aleji ambazo ni nyingi kwa kutegemea eneo husika la mwili, lakini kwa ujumla kama ni mfumo wa hewa ndiyo ulioguswa, mtu anaweza kuwa na matatizo katika kupumua yaani akapata kikohozi au kubanwa na pumzi, makamasi na kuziba kwa pua, muwasho kwenye pua na koo, au kupumua kwa kutoa sauti kama mtu anayepiga filimbi.
allergies-texasLakini kama macho yataguswa, muhusika huhisi hali ya macho kuchoma, kutiririkwa na machozi na muwasho kwenye macho, macho kuvimba na kuwa mekundu na kadhalika.
Iwapo mtu atakula kitu ambacho ana aleji nacho anaweza kuwa na dalili kama vile kuharisha, kichefuchefu, kutapika, kusokotwa au kuumwa na tumbo na hata hali mbaya ya kutishia maisha.
Vinavyosababisha mzio au allergens vinapogusa ngozi vinaweza kusababisha ngozi kuwa na mabakamabaka, kubabuka, kuvimba, muwasho, kuota vipele na malengelenge, michubuko au ngozi kuwa nyekundu.
Aleji zinazohusisha mwili mzima zinaweza kuwa na mkusanyiko wa dalili zote tulizozitaja.
Wakati mwingine aleji inaweza kushadidisha hali ya baadhi ya watu wenye magonjwa kama ugonjwa wa ngozi wa eczema au pumu na kufanya hali iwe mbaya zaidi.
Makala yetu haya yataendelea toleo lijalo.

Leave A Reply