The House of Favourite Newspapers

Fahamu tatizo la uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovarian cyst)-2

mada hii ambapo tuliona uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke.

SASA ENDELEA…

AINA nyingine ya uvimbe ni polycysitic appearing cyst- ambao unakuwa mkubwa na huwa umezungukwa na vijivimbe vingine vidogovidogo na huonekana hata kwa wanawake wenye afya njema au wale wenye matatizo ya homoni. Aina ya sita ya uvimbe ni cystedenoma- ni aina ya uvimbe unaotoka kwenye tishu za ovari na hujazwa na majimaji yenye kuvutika. Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa sana hata kufikia inchi 12 au zaidi kwa upana. Aina ya mwisho ya uvimbe unaowapata wanawake ni endometriomas au endometrial.

SABABU ZA UVIMBE

Vihatarishi vya tatizo la uvimbe kwenye mayai ya mwanamke ni pamoja na historia ya awali ya ovarian cyst. Kwa wanawake ambao wazazi wao au watu wao wa karibu wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo kuna uwezekano mkubwa nao wakapatwa na tatizo hilo.

Sababu nyingine inayoweza kusababisha uvimbe katika mayai ya mwanamke ni kuwa na mzunguko wa hedhi usiokuwa na mpangilio maalum. Kihatarishi kingine ni kuwa na mafuta mengi kwenye sehemu ya juu ya mwili na hii ni kwa wale wanawake wanene. Ugumba na kuvunja ungo mapema ni sababu nyingine ambapo mtoto wa kike hasa anayevunja ungo akiwa na umri wa miaka 11 au chini ya hapo huweza kupatwa na uvimbe katika mayai yake.

DALILI;

Maumivu makali, ambayo hayana mwanzo maalum na yanayochoma. Maumivu hayo yanaweza yakawa yanakuja na kupotea au yakawepo moja kwa moja. Kuhisi tumbo kuwa zito, kujaa au kuvimba, maumivu kwenye matiti na hedhi isiyokuwa na mpangilio maalum na maumivu ya muda mrefu kwenye nyonga wakati wa hedhi na ambayo huweza kuhisiwa sehemu ya chini mgongoni. Maumivu haya yanaweza kuanza muda mfupi tu baada ya kuanza hedhi, wakati wa hedhi au mwisho wa hedhi.

Maumivu ya nyonga baada ya kufanya kazi ngumu, mazoezi au baada ya kukutana kimwili, kuhisi kichefuchefu, kutapika na kutokwa na matone ya damu ukeni. Dalili nyingine ni ugumba na kuhisi uchovu, mabadiliko ya haja ndogo yaani kukojoa mara kwa mara, kujikojolea au kushindwa kutoa mkojo wote kutoka kwenye kibofu cha mkojo wakati wa kupata haja ndogo.

VIPIMO

Mgonjwa kufanyiwa endovaginal ultrasound ambayo hufanywa kwa kuingiza mpira maalum kupitia ukeni na kuangalia mfuko wa uzazi na mayai ya mwanamke. Kwa kutumia kipimo hiki, ni rahisi kwa daktari kugundua kama uvimbe kwenye mayai ni wa aina gani na kujua kama ni maji tu (fluid filled sac) au ni maji pamoja na mchanganyiko wa vitu vigumu kwa maana ya complex au ni vitu vigumu pekee ambapo huitwa completely solid.

MATIBABU

Wanawake wengi wana-fibroids ndogondogo, lakini kwa sababu hazina dalili hawezi kwenda hospitalini na hawa ndiyo siku wakibeba ujauzito uvimbe unaongezeka kwa sababu ya vichocheo kuongezeka.

Uvimbe ambao ni mkubwa wenyewe hutibiwa kwa namna zifuatazo; (hospitalini); Dawa ambazo ni gharama sana, mfano donazol, maskini wengi hawawezi kumudu kununua. Vidonge vya maumivu. Vidonge vya kuzuia damu kama tranexamic acid na dawa za uzazi wa mpango (COCs). Njia ya pili ni operation ambazo nazo zipo za aina nyingi inategemea na uvimbe ukubwa na wingi wake.

Myomectomy hii ni operation ya kuondoa uvimbe mmojammoja bila kuondoa kizazi kwa wale wenye uvimbe mmoja uko sehemu nzuri. Total abdominal hysterectomy. Hii operation inaondoa kizazi chote kama uvimbe umekaa vibaya na viko vingi.

Swali la kujiuliza kwa nini mpaka upate dalili ndiyo uanze kushughulikiwa kutibiwa? Kwa nini ubebe ujauzito huku una uvimbe, kisa bado mdogo? Kumbuka uvimbe huu siyo kansa hivyo ondoa hofu. Mbali na donazole ambayo ni ya gharama na haishauliwi itumiwe kwa muda mrefu kwani inasababisha mwanamke anakua na sifa za kiume.

-MWISHO-

Comments are closed.