Fahyma Afichua Siri Penzi La Rayvanny

Wakati watu wakiendelea kuchonga kwenye mitandao ya kijamii juu ya penzi lake na staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, mama mtoto wake, Fahyma amefichua siri ya uhusiano wao.

 

Fahyma ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, kadiri watu wanavyozusha maneno juu ya kuachana kwao, ndivyo wanalinogesha penzi lao siku hadi siku.

“Dawa ya watu ambao wanasemasema kila wakati, ni kuwadhihirishia maneno yao hayatugusi na kama penzi alilipanga Mungu, ni ngumu sana binadamu kulipangua.

 

Kadiri wanavyosema, ndivyo tunazidi kupeta,” amesema Fahyma ambaye kumekuwa na tetesi za mara kwa mara za kuachana na Rayvanny au Vanny Boy.

Stori:IMELDA MTEMA, Ijumaa

CORONA UPDATE: Wagonjwa wa CORONA Wapungua , Katibu Mkuu Wizara ya Afya ATHIBITISHA…


Loading...

Toa comment