FAHYMA AFUNGUKIA KUKAA UTUPU

Fahyma ‘Mama Jaydan’

MZAZI mwenza wa mkali wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Fahyma ‘Mama Jaydan’ amefunguka juu ya watu wanaomuandama kuhusu mavazi yake ya kuacha mwili wake nusu utupu na kusema ifike wakati wamzoee.  

 

Akizungumza na Zamotomoto, Fahyma alisema kuwa haoni shida ya vinguo vyake ndiyo maana anavivaa kwa sababu kwake ni kawaida na hata watu waliomzoea wanajua kuwa ndivyo alivyo.

 

“Kwani kuna mtu anateseka jamani? Mbona sioni kama ni nguo za kutisha sana za kuwafanya wanijadili? Halafu nilichogundua hao hawajanijua vizuri maana wanaonijua wala hawanishangai kwa sababu wanajua ndizo nguo zangu na napenda fasheni,” alisema Fahyma

Na Shamuma Awadhi, Dar

Toa comment