Fahyma Ana Mimba ya Rayvanny?

BABY mama wa msanii Rayvanny, Fahyma ameendelea kuonesha ishara kwamba huwenda amerudiana na jamaa huyo baada ya kudaiwa kubeba mimba yake.

 

Fahyma anadaiwa kuwa amebeba ujauzito wa mtoto wa pili, lakini inafahamika kwamba hakuna mwanaume mwingine aliye karibu yake zaidi ya Rayvanny ambaye amezaa naye mtoto mmoja.

 

Mrembo huyo ameendelea kuposti picha zikionesha tumbo lake likionesha kwamba ni mjamzito na siyo kwamba ameshiba ubwabwa huku akipokea pongezi kutoka kwa mastaa mbalimbali akiwemo Muna Love.

 

Alichokifanya Fahyma ni kuwashukuru wote wanaompongeza kwa kuwa mjamzito.

Inafahamika kwamba, Fahyma na Rayvanny walitengana mwaka jana baada ya jamaa huyo kutimkia kwa mrembo Paula Kajala ambaye kwa sasa yupo masomoni nchini Uturuki.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR


Toa comment