Fahyma: Natongozwa sana, ila Rayvanny…

 MKE wa msanii wa Bongo Fleva ambaye ni memba wa Kundi la Wasafi Classic Baby ‘WCB’ Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ Fahyma amesema anapata usumbufu wa kutongozwa na wanaume wengi wakimtaka kimapenzi ila kambwe hawezi kumsaliti mumewe.

Akibonga na Za Motomoto ya Risasi, Fahyma ambaye pia ni mwanamitindo alisema kuwa wanaume wengi wamekuwa wakimfuata DM (Direct Message) kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumtongoza bila hata kuogopa kwamba yeye sasa hivi ni mke wa mtu.

“Natongozwa sana na wanaume DM, wengi wananitaka kimapenzi lakini siwezi kuwa nao kwa sababu mimi tayari ni mke wa mtu na nampenda sana mume wangu (Rayvanny), tena sijawahi kufikiria kabisa kumsaliti kwa sababu ananionyesha upendo wa kweli na kunijali pia,” alisema


Loading...

Toa comment