FAHYMA, RAYVANNY WAFUNGA NDOA YA SIRI

Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Fahyma ‘Mama Jayden’

MAMA mtoto wa mkali wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’ Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Fahyma ‘Mama Jayden’ ameweka wazi kuwa yeye na mzazi mwenzie wameshafunga ndoa kwa siri kilichobaki kati yao ni sherehe tu na kufanya watu wengi kupata na maswali.

 

Akibonga na Ijumaa, Fahyma alisema alichokiandika katika mtandao wake kuhusu ndoa yake na mzazi mwenziye huyo ni kweli na siku za hivi karibuni ataweka wazi k uhusu taratibu za sherehe yao.

 

“Nilichokiandika nilikimaanisha kuwa ndoa tumeshafunga kama ambavyo imeonekana kwenye mitandao na kilichobaki ni kufanya sherehe tu ambayo tutatangaza hivi karibuni taratibu zote kwa sababu bado kuna mambo hayajakaa sawa ndio maana hatujaweka wazi kuhusu ndoa tuliyofunga ni ya dini gani na tulifungia wapi yote mtafahamu, lakini kwa sasa siwezi kuzungumza chochote zaidi ya hayo,” alisema Fahyma.

 

Fahyma na Rayvanny ambao wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume, Jayden ambaye ana umri wa mwaka mmoja na miezi kadhaa.

Stori: Shamuma Awadhi.

Toa comment