The House of Favourite Newspapers

Fahyma: Simchukii Paula

0

HATIMAYE Fahyma ameanza kulegea na kukubali yaishe; amebariki laivu penzi la baby daddy wake, Rayvanny na Paula Kajala.

Kwa mdomo wake, Fahyma amesema; “Simchukii Paula hata kidogo…”

 

Fahyma ambaye ni mwanamitindo na mbunifu wa mavazi maarufu Bongo amefunguka juu ya mambo mengi ikiwemo ishu ya kurudiana na Rayvanny wakati huu ambao Paula yupo masomoni nchini Uturuki.

 

Fahyma anasema kuwa, anaheshimu na kumpenda Rayvanny ambaye ni staa wa Bongo Fleva kwani ni baba wa mtoto wake na wanashirikiana kumlea mtoto huyo, lakini haitatokea wakarudiana tena au wakawa kwenye mapenzi.

 

“Rayvanny ni baby daddy wa mtoto wangu, ananiheshimu na mimi ninamheshimu, lakini pia uhusiano wake (na Paula) ninauheshimu sana na siyo adui kabisa.

 

“Na mtu yeyote ambaye atakuwa ni adui wa Rayvanny pia ni adui yangu…” Anasema Fhyma akimaanisha kwamba endapo Rayvanny atapata matatizo, basin a mwanawe atakuwa na wakati mgumu wa kupata matunzo kutoka kwa baba yake.

 

Fahyma anasema kuwa, mwanawe Jaydany anaishi kishua kwa sababu anapata kila kitu kutoka kwa baba yake, Rayvanny.

Kuhusu Rayvanny kudai kwamba amemmisi Paula na kumuita mke, Fahyma anasema kuwa ni haki yake kabisa kwa sababu ni watu ambao wanapendana.

 

Kuhusu mwanawe kwenda kulelewa na Paula, Fahyma anasema anaweza akamchukua kisha akamrudisha kwake, lakini si kumuachia kabisa ili amlee.

“Simchukii Paula na wala siwezi kumchukia…” Anasema Fahyma.

 

Kabla ya kutengana mwaka jana, Fahyma na Rayvanny walidumu kwenye mapenzi kwa miaka saba na kujaaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jaydany kabla ya jamaa huyo kunyakuliwa na Paula.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply