The House of Favourite Newspapers

FAIDA 8 ZA KULA CHAKULA PEKE YAKO

 

Sio kila mmoja hufurahia kula peke yake,Baadhi ya watu hawapendelei kula peke yao huku wengine wakihofia huenda wakijihisi upweke kiasi cha kupoteza hamu ya kula chakula.

 

Uchunguzi mdogo umebaini kwamba kuna faida ndogo za kufikirika endapo utakula peke yako bila kuwa na mtu yeyote maeneo uliyopo.

 

1.Unaweza kula popote unapotaka.

 

Kula peke yako hukufanya kujisikia huru kula chochote unachotaka bila kuwa na hofu watu wengine wanataka kula nini.

 

Pia unaweza kuchagua ulie mahali gani(chumbani, jikoni, chooni,chumbani na kwingineko) kwasababu kila binadamu ana tofauti yake.

 

Pengine wewe hupendelea viungo tofauti ambayo huenda ikawakwaza watu wengine, kwa mfano samaki wa kusindikwa ana harufu kali japo ni mlo maarufu nchini Uswidi.

 

Au pengine wewe unapendelea vyakula vya wanga na pia huoni tatizo kula viazi vingi vilivyochanganywa na pasta.

Bila shaka kama hakuna mtu wa kukuchagulia kile utakachokula utakuwa huru kuamua chochote utakacho bila hofu.

 

Uzuri wake ni nini? Unaweza kuwa mbunifu kwa kuchanganya vyakula tofauti bila kumkwaza mtu mwingine endapo mchanganyiko huo utakuwa na muonekano mbaya.

 

2.Huna haja ya kuomba chakula cha mwenzako

 

Ushawahi kujikuta umeagiza chakula kitamu ambacho huenda umekitamani kwa miezi kadhaa ukapata rafiki zako wote wanataka kukionja mpaka unaishia kula kijiko kimoja?

 

Huenda ni vyema kula na wenzako lakini watu wengine hawapendelei kwa mfano kupoteza 20% mnofu samaki ili kuonje kijiko kimoja cha umma cha pie ya samaki.

 

Kula peke yako wakati mwingine hukupatia utulivu, na wakati mwingine mfanya mlaji kula chakula chote bila kupeana.

 

3.Humsaidia mtu kuzingatia lishe bora

 

Ikiwa unajaribu kufuata utaratibu fulani walishe bora, kula peke yako hukusaidia kuzingatia utaratibu huo.

Utafiti uliyowasilishwa kwa chama cha masuala ya moyo cha Marekani unaashiria kuwa 60% ya watu wanaojaribu kula lishe bora hubadili mkondo huo wanapojumuika na kula na watu wengine.

 

Utafiti mwingine uliyofanywa na wanafisiolojia wa chuo kikuu cha jimbo la Georgia umeonesha kuwa kula pamoja kwa vikundi huchangia watu kula 44% zaidi, ikiwa ni pamoja na kula kiwango cha juu cha vyakula vilivyo na mafuta mengi.

 

4.Unaweza kula kwa nafasi yako

 

Utafiti unaashiria kuwa mwenendo wa mtu wa kula chakula hutegemea na watu anaotangamana nao.

Kwa kula peke yako, huenda ukajiamulia ni wakati gani wa kula na kiasi ya chakula unachotaka kwa wakati huo.

 

Kuwa muangalifu kula chakula huku ukiwa unatazama televisheni- filamu za kusisimua humteka mtu mafikira hali ambayo imetajwa kuwafanya watu kula chakula kingi zaidi.

 

5.Inakupatia nafasi ya kuangazia ladha ya chakula

 

Kula peke yako hukusaidia kuangazia kwa makini kile unachokula.

Hii inamaanisha kuwa unaweza kuchukua muda wako kufurahia ladha ya chakula badala ya kumsikiliza mtu fulani kwa mfano akizungumzia gari lake jipya.

 

6.Unaweza kula katika madhari ya kupendeza huku ukifurahia mazingira yako.

 

Huenda ukachukua muda kuzoea kula peke yako, lakini ukizingatia mambo yanayofanyika katika ulimwengu wa sasa huenda ni wazo zuri kula kimya subuleni mwako ukifurahia filamu upendayo.

Migahawa yenye shughuli nyingi wakati mwingine huwafanya watu kupoteza muda kutafuta mahali pa kukaa huku wengine wakiamua kukaa karibu na kaunta na kuacha viti visivyo na watu.

Ikiwa unahofia huenda ukaonekana mpweke usijali: visa vya watu kula peke yao vimeongezeka kila pembe duniani – kwa mfano: 87% ya waingereza wanasema kuwa wanafurahia kula peke yao.

Mwaka 2015 utafiti uliyofanywa na OpenTable – huduma ya kimataifa ya mgahawa mtandaoni ulibaini kuwa watu wengi zaidi wamekuwa wakiagiza huduma ya kibinafsi badala ya pamoja katika kipindi cha miaka miwili, kwa hivyo huenda akajipata si wewe peke yako unafurahia kula mwenyewe.

 

7.Hutalazimika kuwasikiliza watu wengine wakitafuna chakula

 

Ikiwa hupendi kusikia sauti ya watu wakitafuna chakula sasa una nafasi ya kulapeke yako kwa amani.

Hali ya kusumbuliwa na sauti ya mtu akitafuna chakula hujulikana kama misophonia -kunawatu hawapendi kabisakusikia sauti ya mtu akitafuna chakula.

Haijabainika hali hiyo ni mbaya kiasi gani na endapo inaweza kutibiwa.

 

8.Unaweza kula wakati wowote popote unapotaka

 

Ukiwa peke yako unaweza kula wakati wowote wa siku kuanzia alfajiri, hali ambayo inakupatia uhuru wa kuamua kile unachopenda.

 

Hata hivyo wataalamu wa masuala ya lishe wanashauri ujiepushe na kula vyakula vilivyo viungo vikali nyakati za asubuhi kwani huenda ukasalia na harufu ya vyakula hivyo siku nzima.

Bila shaka hungependelea kuingia mkutano wa kazini asubuhi ya Jumatatu ukinukia kitungu saumu.

 

#ISIKUPITE : MASTAA 10 WENYE MKWANJA MREFU BONGO!

 

Comments are closed.