The House of Favourite Newspapers

Fainali ya FA: Yanga vs Azam FC kupigwa Zanzibar

0

Fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB ambayo itawakutanisha Mabingwa watetezi, Yanga Sc dhidi ya Wanalambalamba, Azam Fc imehamishiwa Uwanja wa New Amaan, Zanzibar badala ya Babati mkoani Manyara

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya baadhi ya miundombinu muhimu mjini Babati kutokuwa tayari kwa ajili ya fainali hiyo pamoja na sababu za kiusalama.

TFF imezishauri Mamlaka za mkoani Manyara kuendelea kufanya marekebisho katika miundombinu hiyo ifikiriwe kwa ajili ya fainali zijazo na michuano mingine mikubwa.

Leave A Reply