The House of Favourite Newspapers

Faini Milioni 2 Ukikaidi Kuvalisha Mifugo Yako Hereni za Kielektroniki Kabla ya Desemba 10

0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Tixon Nzunda

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imewataka wafugaji wote nchini kuhakikisha mifugo yao inatambuliwa kwa kuvalishwa hereni za kieletronic kabla ya tarehe 30 mwezi wa kumi na watakaokaidi agizo hilo watalipishwa faini ya shilingi millioni mbili.

 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo inayesimamia Sekta ya ufugaji alipotembelea Ranchi ya Taifa ya West Kilimanjaro iliyopo Wilayani Hai mkoani hapa ambapo amewataka wafugaji kuwavalisha hereni za kieletronic mifigo yao kwa kuwa itawasaidia kuuza mifugo yao katika masoko ya kimataifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ranchi za Taifa Peter Lawrence Msofe

Katibu huyo amesema wafugaji watakaokaidi agizo hilo Serikali itawachukulia hatua kama anavyobainisha pia aliweza kukutana na kutoa elimu kwa wafugaji waliopanga maeneo ya malisho katika Ranchi ya Taifa ya West Kilimanjaro ambapo wafugaji hao waliweza kutoa kero na maoni yao.

 

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ranchi za Taifa Peter Lawrence Msofe amesema Bodi ya Ranchi za Taifa wameamua kufanya mabadiliko ya ufugaji lengo likiwa ni kuhakikisha wanakuwa na vituo vya umahiri katika uzalishaji.

Mifugo

Hata hivyo Wizara ya Mifugo na Uvuvi imedhamiria kuhakikisha wafugaji nchini wananufaika na mifugo wanayoifuga na kuzisimamia Ranchi za taifa kuwa mfano katika uzalishaji.

Leave A Reply