Faiza Aanika Alivyoikwepa Corona China

STAA wa filamu ya Baby Mama Bongo, mjasiriamali Faiza Ally amefunguka alivyofanikiwa kurejea nchini akitokea nchini China na kuhofiwa kupata maambukizi ya Virusi vya Corona vinavyosambaa duniani kote.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Faiza alisema, akiwa nchini humo alijilinda kwa kila namna kwani alikuwa akiogopa kufa kwa sababu ana watoto na ndugu wanaomtegemea.

“Unajua watu wanadhani mimi ni mjinga au sipendi familia yangu kwa hiyo hata nilivyoondoka watu wakasema sana, lakini ukweli ni lazima niwajibike na pia kujilinda sana na ninaamini Corona itaniepuka tu,” alisema Faiza ambaye mbali na sanaa ya uigizaji huwa ni mjasiriamali anayefuata mizigo nchini China na kuzileta Bongo.

Stori: Imelda Mtema, Dar


Loading...

Toa comment