The House of Favourite Newspapers

FAIZA AIBUKA NA WANAOONGEZA MAKALIO

Faiza Ally

KAIBUKA! Mwanadashoti wa Bongo Movies asiyeishiwa vituko, Faiza Ally ameibuka na stori ya wanawake wanaoongeza shepu za miili yao hasa makalio, akiwaomba kuacha kwani ni ukosoaji wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Faiza ambaye pia ni mfanyabiashara alisema hakuna jambo ambalo halipendi kama mtu kumuagiza dawa za kufanya mabadiliko kwenye mwili hivyo anawasihi wanawake wajikubali kama walivyoumbwa.

“Sipendi wanawake kutojikubali. Mimi siwezi kumletea mtu dawa ya kuongeza makalio maana naona kama si za kweli, lakini pia ni vyema kujikubali, hicho ndicho kitu muhimu,” alisema Faiza anayeagiza bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Comments are closed.