FAIZA: MTANIONA CHIZI, ILA BAADAYE MTANIELEWA

Faiza Ally

MSANII wa filamu na pia mzazi mwenzie na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’ Faiza Ally amefunguka kuwa watu wengi wanaweza wasimuelewe kwa jinsi anavyopigana na maisha ili tu kutimiza ndoto yake ila ipo siku wataelewa.  

 

Akizumgumza na Ijumaa, Faiza alisema anakesha China, kubeba mizigo ya watu waliyomuagiza vitu kwa sababu anatafuta pesa na nia yake kubwa ni kuwa tajiri tena kwa kutafuta kwa jasho.

 

” Naona watu hawanielewi mimi ni kukesha na kubeba mizigo ya watu walioaniagiza ni kwa sababu nausaka utajiri tena siyo hela ya haramu ni ya jasho langu na ninataka kuonyesha watu inawezekana na ipo siku watanisimulia tu” alisema Faiza.

 

Faiza hivi sasa yupo nchini China, kwa ajili ya kufanya biashara ambapo watu wanamuagiza vitu mbalimbali na yeye anavituma kutoa kule kuja nchini Tanzania

Stori: Imelda Mtema

Toa comment