The House of Favourite Newspapers

Familia imebariki penzi la Naj na Baraka – Lady Naa

0

BARAKA NA NAJY (3)Baraka Andrew ‘Baraka The Prince’ na mpenzi wake Najma Dattan ‘Naj’.

Stori: Hamida Hassan, Wikienda

DAR ES SALAAM: Dada wa msanii wa Bongo Fleva, Najma Dattan ‘Naj’ ambaye ni mtangazaji, Nasra Rajesh ‘Lady Naa’ amefunguka kuwa familia yao imelibariki penzi la binti yao huyo na mwanamuziki mwenzake, Baraka Andrew ‘Baraka The Prince’ kwani wamegundua ndiye mwanaume sahihi kwa mtoto wao.

BARAKA NA NAJY (1)Lady Naa aliliambia Wikienda kuwa Naj amewahi kutoka na wanaume kadhaa wakiwemo mastaa wa Bongo Fleva, Herry Sameer ‘Mr Blue’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ lakini hakuna aliyewahi kuwa na penzi la kweli kwake kwa kumweka kwenye mstari na kumpenda kama ilivyo kwa Baraka.

lady naaLady Naa.

“Wazazi wamemkubali Baraka kwa sababu hanywi pombe wala havuti sigara. Ni mshauri mzuri wa Naj kwani amefanikiwa kumfanya aache sigara, ishu ambayo ilikuwa inawaumiza sana wazazi wake,” alisema Lady Naa.

Ukiacha figisufigisu za hapa na pale, kwa sasa penzi la Naj na Baraka ndiyo habari ya mjini kufuatia mahaba wanayooneshana popote wanapokuwa.

Leave A Reply