Familia Marathon 2021 Kutimua Vumbi Jumamosi Desemba 11

Mwenyekiti wa mbio za Familia Marathon 2021, Bi. Francisca Alphonce (wa tatu Kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Disemba 11, jumamosi. Wengine ni wawakilishi wa Kampuni zinazodhamini mbio hizo.

Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya KCB, Christina Manyenye (wa nne kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu udhamini wao katika mbio za Familia Marathon 2021 zinazotarajiwa kutimua vumbi lake jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii. Usajili unaendelea kufanyika katika Tawi la KCB Mlimani City.

Waandaaji na wadhamini wa Familia Marathon 2021 wakionyesha kwa waandishi habari, Dar es Salaam leo, medani na baadhi ya zawadi watakazopewa washiriki wa mbio hizo zitakazofanyika kwa mtindo wa kutembea na kukimbia jijini humo jumamosi wiki hii. Mbio za mwaka huu zimedhaminiwa na  KCB Bank, KP Motors, UTT Amis, Premier Security, Optical Centre, Rani Sanitary Pads, Planet Fitness, Knight Support na Xpress Rent.

 


Toa comment