The House of Favourite Newspapers

FAMILIA: MASOGANGE ATAAGWA KESHO JUMAPILI LEADERS

Msanii aliyekuwa akipamba video za muziki (video queen), Agnes Gerald ‘Masogange’ enzi za uhai wake. BAADA ya wadau wa sanaa kukaa na familia kujadili ratiba ya mazishi ya Agnes Gerald (Masogange), wameamua mwili wa marehemu utaagwa kesho (Jumapili) katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam ambapo pia patafanyika misaa maalum na Shughuli hiyo itaanza saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Emma Gerald, Dada wa Agnes Masogange, baada ya hapo mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Mbeya kwa ajili ya mazishi ambapo pia kutakuwa na mabasi maalum mawili kwa wale watakaopenda kumsindikiza marehemu mpaka Mbeya.

 

“Tutaaga kesho asubuhi saa 3 pale Leaders, na kisha tutasafirisha kuelekea Mbeya kwa mazishi”, amesema Emma.

Comments are closed.