The House of Favourite Newspapers
gunners X

Familia: Nandy Hakai na Nenga

0

UNAAMBIWA licha ya kwamba staa wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ kuoneshana mahaba mazito hadharani na mchumba wake wa siku nyingi, William Lyimo ‘Billnass’ au ‘Nenga’, lakini kumbe hawakai pamoja.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA mmoja wa wanafamilia wa Nandy ambaye aliomba hifadhi ya jina anasema kuwa, hapo katikati ni kweli wawili hao walitengana kwa sababu wanazozijua wenyewe, lakini baadaye walipatana hadi kufikia hatua ya kutengeneza wimbo wa pamoja.

 

“Nandy na Billnass waligombana hapo katikati ndiyo maana mlikuwa hamuwaoni pamoja, lakini hawa watu wanapendana bwana, walikaa chini wakayamaliza ndiyo hadi wamefikia hatua ya kutoa ngoma ya pamoja, lakini unaambiwa kipindi wamegombana, ndiyo walitengana kwa sababu ilimbidi Billnass akaishi sehemu nyingine.

 

“Na kama mnataka kupata ukweli wote ninyi mtafuteni ndugu yake yeyote yule ataawaambia,” anasema mtu huyo.

Kama kawaida ili kupata ukweli wote, Gazeti la IJUMAA liliingia kazini na kufunga safari hadi Mbezi-Beach jijini Dar zilipo ofisi za Nandy Bridal ambapo baada ya kubisha hodi alitoka kijana mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mfanyakazi wake na mazungumzo yalikuwa hivi;

 

IJUMAA: Mambo vipi?

KIJANA: Safi, niwasaidie nini?

IJUMAA: Tuna shida ya kumuona Nandy au Billnass, tumewakuta?

KIJANA: Ninyi ni kina nani?

IJUMAA: Sisi ni waandishi wa Gazeti la IJUMAA (waandishi wanatoa vitambulisho vya kazi na kumuonesha kijana; kijana naye anaonekana kuwaamini na kuanza kuwapa ushirikiano).

KIJANA: Sasa Nandy haishi hapa, hii ni ofisi yake, labda ngoja niwape namba ya mtu wake wa karibu (dada yake Nandy) ili muwasiliane naye.

IJUMAA: Sawa haina shida (kijana anatoa namba ya mtu huyo na mazungumzo yanakuwa hivi);

MWANDISHI: Habari yako?

Dada wa Nandy: Salama, naongea na nani?

Mwandishi: (mwandishi wetu anajitambulisha kisha wanaendelea na mazungumzoi) tupo hapa Nandy Bridal tuna shida ya kuonana na Nandy au Billnass kwa ajili ya mahojiano…

DADA WA NANDY: Ahaa, sasa huyo kijana mnayehitaji kumuona (Billnass) wala haishi na Nandy kila mmoja anaishi kivyake, lakini pia Nandy huwa hakai hapo ofisini mara kwa mara ndiyo maana hamjamkuta.

MWANDISHI: Kwa nini unasema hawaishi pamoja wakati mwanzo walikuwa wanakaa wote?

DADA WA NANDY: Wale ni wachumba, hawajafunga ndoa bado, lakini nadhani jibu zuri la swali lenu wanalo wao wenyewe hivyo mkiwatafuta itakuwa vizuri.

MWANDISHI: Asante sana.

DADA WA NANDY: Karibuni sana.

Mwaka 2016, wawili hao waliingia kwenye mahaba mazito, lakini baadaye wakaja kutengana, miaka ikakatika huku kila mmoja akiwa ameanzisha uhusiano mpya na mtu mwingine, mara paap tukashangaa kuwaona tena wamerudiana na penzi lao kutaradadi.

Raha zikamnogea mtoto wa kichaga, Billnass akaona isiwe taabu, wakati mrembo Nandy akitumbuiza kwenye kipindi kimoja maarufu mara ghafla usiku wa manane, Nenga akamfanyia surprise ya maana kwa kumvisha pete ya uchumba ambapo mpaka sasa mashabiki bado wanasubiria kuona wakifunga ndoa takatifu.

Leave A Reply