The House of Favourite Newspapers

Familia ya Diamond Yamuumiza Mtoto wa Hamisa, Yamtelekeza Kizembe

0
Hamissa Mobetto akiwa na mwanaye Dylan

DYLAN; ni mtoto mwingine wa kiume wa staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz ambaye amezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

 

Leo Jumatatu Agosti 8, 2022 ni birthday ya mtoto huyo, lakini kinachoshangaza familia ya Diamond haijafanya chochote, badala yake bado wapo nchini Afrika Kusini ambako wikiendi iliyopita walimfanyia birthday ya kufuru mtoto mwingine wa jamaa huo, Tiffah Dangote aliyezaa na Zari The Boss Lady.

 

Hadi jioni hii, Diamond hajaposti, Mama Dangote hajaposti, Machawa wa Wasafi hawajaposti, ni WasafiTV pekee ndiyo wameposti.

Diamond Platnumz

Ishu hiyo inasemekana itakuwa inamuumiza mno Hamisa na mwanawe huyo kisaikolojia huku bado kukiwa na zile tetesi kwamba hawaamini kama Dylan ni mtoto wa Diamond kwa kigezo cha kutofanana.

 

Hata hivyo, kinachofahamika ni kwamba, walishafanya mpaka DNA na majibu wanayo, lakini ifike mahali Diamond atambue kwamba kutofanana na mtoto siyo sababu ya kudai mtoto siyo wake.

Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply