The House of Favourite Newspapers

Familia Yathibitisha Nemes Tarimo Kufia Vitani Nchini Ukraine, Yafunguka – Video

0
Nemes Tarimo enzi zauhai wake.

Taarifa za kifo cha Raia wa Tanzania, Nemes Tarimo, zilisambaa pamoja na video ikionesha akiwa anaagwa kwa heshima na vikosi vya jeshi nchini Urusi.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa Tarimo, alikamatwa kwa kesi ya dawa za kulevya kisha akafungwa, baada ya muda alipatiwa taarifa za kujiunga na kundi la Wagner na kuahidiwa kuachiwa huru baada ya miezi sita ya kupambana katika uwanja wa vita.

‘’Alitupatia taarifa kuwa anajiunga kwenda kwenye vita dhidi ya Ukraine, tulimsihi sana asijiunge lakini akasema huwezi jua nitapata uhuru wangu kwa hiyo akajiunga na mara ya mwisho kuwasiliana ilikua Oktoba 17 na hakupatikana tena, ’’anasema ndugu wa Nemes ambaye hakutaka jina lake

Nemes alienda Urusi kwa ajili ya masomo ya shahada ya uzamili katika Chuo cha Teknolojia cha Urusi, MIREA.

Familia ya Nemes Tarimo imethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuwa wanasubiri mwili wa mpendwa wao kwa ajili ya Maziko.

Kwa mujibu wa familia, Tarimo alifariki mwishoni mwa mwezi Oktoba na kwamba taarifa ya kwanza walipatiwa na marafiki wa karibu mwishoni mwa mwezi Desemba kuwa kijana wao amefariki. Baadaye walipata taarifa rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania huko Moscow.

Baada ya kupokea taarifa za kifo chake, ilikua ngumu kwa familia kuamini taarifa hizo, lakini baada ya video ya kuagwa kwakwe kusambaa ndio walianza kuona kuwa kweli kijana wao amefariki.

‘’Kwakweli hatukuamini kabisa, lakini baadae video ikaanza kusambaa na kuangalia majina yake yote matatu ni sahihi ndio tukajua kweli kijanza wetu ametutoka, lakini bado hatuamini hadi tuone mwili wake’’ anasema mama mlezi wa Nemes.

Mwili wa Tarimo ilikua urudishwe wiki kadhaa zilizopita lakini hadi sasa bado familia haijapokea mwili huo.

Leave A Reply