The House of Favourite Newspapers

Familia yatinga Hospitali ikidai pesa

0

IMG_0630Watoto wa familia ya mzee Michael Mgunda (72) wakiwa nje ya Kituo cha Afya cha Mselem (Mselem Medical Center), Kipunguni, Dar 

Stori: Chande Abdallah na Suzan Kayogela
WATOTO wa familia ya mzee Michael Mgunda (72) wametinga katika Kituo cha Afya cha Mselem (Mselem Medical Center), Kipunguni, Dar wakidai kudhulumiwa gharama za matibabu za mgonjwa wao mzee huyo mwenye tatizo la kibofu cha mkojo.

IMG_0637Watoto wakiwa na mzee Michael Mgunda wakifanya mahojiano na mwandishi wetu.

Tukio hilo lilijiri Novemba 11, mwaka huu ambapo ndugu hao walidai awali walimpeleka mgonjwa wao katika kituo hicho ili afanyiwe operesheni lakini walishangaa wakitozwa gharama nyingi ikiwa pamoja na nyingine zisizo na maana lakini mgonjwa wao hakutibiwa.

IMG_0631Gharama walizolipia katika Kituo cha Afya cha Mselem (Mselem Medical Center)

Akizungumza na Amani, mtoto wa mzee huyo, Rashid alisema moja kati ya gharama walizodai kutozwa kiholela ni mgonjwa wao kuwekewa dripu nne, kuchomwa sindano mbili ambazo zinadaiwa hazikuhusika na tatizo la mgonjwa huku akiachwa bila kufanyiwa upasuaji.

“Gharama zote zilifika shilingi laki moja na elfu sitini na saba (167,000). Nilishangaa siku ya pili nakwenda kumchukua mgonjwa namkuta akiwa katika hali mbaya halafu hajafanyiwa upasuaji. Nikamfuata daktari kumuuliza lakini hakunipa majibu sahihi, ndiyo nikataka nirudishiwe gharama zangu,” alisema Rashid.

Hata hivyo, alidai wakati anafuatilia fedha zake alizungushwa kwa muda wa siku tano akiambiwa angerudishiwa shilingi 50,000 tu tena kwa njia ya mtandao ambapo alidai hajapata fedha hizo mpaka hivi karibuni (alipozungumza na gazeti hili) huku wakilazimika kumpeleka mgonjwa wao Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alitibiwa kwa shilingi elfu 50,000.

IMG_0620Rashid alisema kutokana na hali hiyo, alikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Stakishari na kupatiwa namba ya jalada STK/RB/14318/15 KUJIPATIA PESA KIDANGANYIFU.

Amani liliwatafuta wahusika wa hospitali hiyo ambao walikiri kumpokea mgonjwa huyo tarehe husika na kutomfanyia operesheni lakini walisema wameshamlipa Rashid kiasi hicho cha pesa alichokuwa akidai lakini wanashangaa akiendelea kuwadai.

“Huyu mgonjwa tunamjua lakini hayo madai ya mtoto wake kuwa hatujamlipa si ya kweli. Tulishamlipa kwa mtandao na meseji tulimuonesha. Sasa kwa nini hakubali hilo, tunashangaa anakuja na RB ambayo pia tuna shaka nayo,” alisema mtunza fedha wa kituo hicho, Mwanahawa Ali.

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS

GLOBALBREAKINGNEWS100.jpg

Leave A Reply