The House of Favourite Newspapers

Familia Yawasamehe Wote Waliomkosea Ruge – Video

FAMILIA ya marehemu Ruge Mutahaba imesema imewasamehe watu wote waliomkosea au kutoelewana na ndugu yao wakati akiwa hai kwani ni hali ya kawaida kwa binadamu.

Hayo yamesemwa leo Machi 2, 2019 na mtoto mkubwa wa marehemu Ruge aitwaye Mwachi Mutahaba wakati akitoa wasifu wa baba yake katika Viwanja vya Karimjee kabla ya kumuaga kwa safari ya Bukoba kwenda kuzikwa.

Akizungumza mbele ya Rais Magufuli na viongozi wengine, ndugu, jamaa na marafiki,  alitoa msamaha huo kwa niaba ya familia yake.

“Wapo waliomkosea Ruge na pengine wapo wanaoendelea kumkosea. Familia imewasamehe wote, tuendelee mbele,” alisema kwa majonzi kijana huyo.

VIDEO: MSIKIE MWACHI AKIZUNGUMZA

Comments are closed.