The House of Favourite Newspapers

Familia yazuia Khloe kurudiana na Lamar

0

LOS ANGELES, Marekani
MODO kiwango, Khloe Kardashian, aliufungua moyo wake na kumsaidia aliyekuwa mumewe, Lamar Odom, Oktoba mwaka jana alipopoteza fahamu lakini sasa mrembo huyo anaonekana kuwa tayari kurudisha penzi kwa staa huyo wa zamani wa NBA lakini tatizo lipo kwa familia yake na marafiki.
Khloe, 32 na Lamar, 36, ni mke na mume lakini waliachana bila talaka mwaka jana kabla ya mrembo huyo kutua kwenye mikono ya mkali wa Hip Hop, French Montana kisha James Harden anayekipiga Houston Rockets inayoshiriki Ligi ya Kikapu ya Marekani (NBA).
Lakini ‘big news’ kwa sasa ni Khloe kudaiwa kuwa yupo tayari kurudiana na Lamar baada ya kuachana na James lakini tatizo lipo kwa marafiki na familia yake ambayo inadaiwa kutopendezwa na suala hilo.
“Marafiki zake na familia wanaona kuwa atafanya makosa akirudiana na Lamar,” kilisema chanzo.

Leave A Reply