The House of Favourite Newspapers

Fanya Haya Kabla ya Kusema; Mwanaume Hata Umpe Nini Haridhiki

0

MUNGU ni mwema. Ijumaa nyingine tunakutakana hapa. Tunapeana elimu ya uhusiano. Kwa wale wanaoamini katika kujifunza kitu kipya kila siku, nawakaribisha tuwe pamoja.

Kama mada inavyojieleza hapo juu, leo tunajifunza kuhusu tabia. Tutaangalia hulka au tabia kwa upande wa wanaume na wanawake. Kizazi cha sasa, kuna desturi imejengeka kwa wanaume na wanawake. Mwanaume anaoa, lakini nje anakuwa na wanawake wengine.

Mwanaume anaweza kuwa ana mchumba ambaye amempa nafasi kubwa ya kuja kuwa mke lakini pembeni anakuwa na mabinti wengine. Hao mabinti anasema ni wa kuzugia. Anawaeleza kabisa kwamba ana mchumba.

Wale mabinti nao wanakubaliana na hali hiyo. Wanakubali kuwa viburudisho wa muda. Wanajua wenyewe wanachokipata. Yawezekana ikawa ni fedha au tu kuridhishwa kimapenzi. Wanawake hao huwa wanakuwa na mbwembwe kwelikweli.

Wanakaba kuhakikisha wanapata wanachokitaka. Matokeo yake humsababishia mwanaume apoteze uelekeo kwa mchumba au mkewe. Kinachotokea huwa ni ugomvi. Wanaharibu uchumba au ndoa za watu.

Hali hiyo ndiyo inayoleta misemo ya wanawake wengi; kwamba mwanaume hata umpe nini haridhiki, wasimuone mrembo barabarani watamtamani.

Mwanaume anajengewa taswira kwamba hata apewe kila kitu na mkewe bado atachepuka. Uchepukaji kwa mwanaume unafanywa kuwa jambo la kawaida. Mwanaume hata akioneshwa ufundi vipi na mkewe, bado atakwenda nje.

Wanawake wenyewe wanahalalisha. Utawasikia wakiambizana mitaani; ‘mwanaume ni wako akiwa kwako, akitoka si wako.’ Eti mwanamke anakuwa na uhakika na mwanaume pindi tu anapokuwa naye nyumbani.

Wanawake hapo hawatumii tena nguvu nyingi kutetea penzi lao, wanaamini hata wakitetea vipi, bado wanaume wataenda nje.

INATOSHA KUISHIA HAPO?

Haitoshi kuishia hapo. Kuna kitu cha kufanya zaidi ya kutoa kauli hizo. Kuna kitu mwanamke unapaswa kujitathmini na kujisahisha kabla ya ‘kujiua’ na kauli hiyo.

CHUKUA ELIMU HII

Wewe mwanamke; kabla ya kufikia hatua ya kusema mwanaume hata umpe nini haridhiki, hakikisha kwanza unamridhisha muwapo faragha, acha gubu, kisirani, usipende kuongea sana na kukuza mambo, mfariji mumeo na mdekeze.

Acha visingizio anapokuhitaji faragha, unamtoa mwenzako kihisia. Unadai hela za matumizi ya kesho yake, unalalamika jana umepewa hela ndogo, unaeleza shida za nyumbani kwenu. Hilo ni tatizo!

Hakikisha mumeo ‘anainjoi’ kuwa na wewe. Usitoe mwanya wa kitu anachokipenda aende kukipata sehemu nyingine.

Kuwa mbunifu faragha. Mjulie mapigo anayoyapenda, muoneshe kwamba unayaweza na ukifanya hivyo kwa asilimia mia moja utakuwa na nafasi kubwa ya kunusuru penzi lako kuliko kuridhika na msemo wa ‘mwanaume hata umpe nini haridhiki.’

Leave A Reply