The House of Favourite Newspapers

Fanya Hivi Kuepuka Kuolewa/ Kuoa Usiyempenda!

0

stress-women-03  Mada ya leo kwenye kilinge chetu cha XXLove inazungumzia kuepuka kuolewa au kuoa mwanamke ambaye humpendi kwani ukifanya makosa basi ndoa itakushinda na kila siku kwako itakuwa ni majuto.

stress-women-01

Najua yawezekana wewe ni miongoni mwa watu ambao mwaka 2017 ulitamani au umepanga kuoa au kuwa na mwenza wako. Ni jambo zuri sana kiimani kwani linakufanya uepukane na mambo ya uzinzi kwa mtu mwenye hofu.

Lakini nakusihi kama utakosea kuoa au kuolewa, hakika utajuta sana katika maisha yako, kwani unayemuoa au kuolewa naye ni mtu ambaye muda mwingi wa maisha yako utakuwa uko naye hivyo ni vyema zaidi ukawa makini katika kumchagua mtu huyo. Kwa akili na macho ya kibinadamu ni ngumu zaidi kumfahamu mwanaume au mwanamke ambaye anakufaa zaidi katika maisha yako lakini ukimshirikisha Mungu kwa maombi ya kweli, hakika hutajuta kamwe kwenye ndoa yako.

Mapenzi ni kitu kimoja ambacho ni sensitive (nyeti) sana hivyo unahitaji umakini wa hali ya juu wa kuchagua penzi au mpenzi kama vile mtu unavyoshauriwa kutunza mboni ya jicho, masikio au kinywa chako.

Unatakiwa kuwa makini katika kuchagua mtu wa kukupa raha maishani mwako maana siyo kila mtu atakupa raha.

Watu wengi wamekuwa wakijilaumu kwa kukosea kuchagua kuoa au kuolewa. Yapo mambo ambayo unaweza kuyafanya ili kuepukana na kuolewa au kuoa mwanamke ambaye humpendi;

 KUPENDA GHAFLA

Kuna baadhi ya watu huwa wana tabia ya kujifanya wanajua kupenda ghafla, wengine wanaitwa malimbukeni, yaani unakuta mtu kamuona mwanaume au mwanamke siku moja (first sight) basi anajifanya kuzuzuka weee!

Hilo ni tatizo kwani unampenda mtu kwa haraka na kuchukua uamuzi wa haraka bila hata kumchunguza na wewe kujichunguza kama ni kweli unampenda mwanamke au mwanaume huyo.

Kwa kuwa umezidiwa na mapenzi feki, ya muda mfupi unakurupuka na kuamua kufanya mipango ya harakaharaka na kwa nguvu nyingi ili utangaze ndoa na kweli unafanikiwa kutangaza ndoa bila kujua kuwa mtu ambaye umempapatikia siyo chaguo lako ila unaongozwa na mihemko ya muda mfupi. Ukisikia kupatwa kwa mapenzi ndiyo huko!

Mara nyingi hii huwatokea watu ambao wanakuwa wanatoka sehemu moja na kwenda nyingine, akikutana na wapenzi wa eneo husika huona kama ni wapya na kujitumbukiza bila kujua tabia zao.

Ukiwa na tabia ya namna hii ni rahisi sana kuolewa au kuoa mwanamke ambaye hukumpenda na mwisho wa siku utalia na kujilaumu mwenyewe kuwa hujihisi raha unapokuwa na mpenzi wako, mara oooh! Sina hamu naye.

Mpenzi msomaji usikose mwendelezo wa mada hii wiki ijayo, kwa maoni na ushauri tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook, Insta:mimi_na_uhusiano au jiunge na M&U WhatsApp kwa namba zilizopo juu.

Leave A Reply