The House of Favourite Newspapers

Farid Mussa aondoka Azam, Kavumbagu kazi ipo

FARIDNa Nicodemus Jonas

Dar es Salaam

AZAM FC inalazimika kubadili mfumo wake, kwani winga wake Farid Mussa amepata timu Denmark, hivyo anaondoka lakini Didier Kavumbagu bado mambo yake ni magumu.

Kocha wa Azam, Stewart Hall, ameiambia Championi Jumamosi: “Niwe muwazi kuhusu kinachoendelea kikosini, asilimia 95 nitampoteza Farid Mussa kwani amepata timu Denmark.

“Anatakiwa akafanye majaribio lakini kutokana na uwezo wake, naamini atasajiliwa moja kwa moja, hivyo hapa nina kazi ya kubadili mfumo wa timu ili mambo yaende sawa.”

Kwa kawaida, Mussa hucheza winga ya kushoto katika kikosi cha Azam na Taifa Stars, hivyo Hall kuelekea mechi dhidi ya Simba Desemba 12, mwaka huu anatakiwa kubadili kitu fulani katika mfumo ili mambo yaende.

Wakati huohuo, straika wa Azam aliyekuwa na mpango wa kwenda Sweden kufanya majaribio, Kavumbagu, mambo yake yamekwama kidogo kwani imekuwa kimya hadi sasa.

Hall alisema kama mambo ya Kavumbagu yataendelea kuwa kimya, atabaki klabuni hapo kushiriki msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano mingine ambayo timu hiyo inashiriki.

Comments are closed.