Fastjet kuisafirisha Taifa Stars kwenda Algeria

 Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu timu ya taifa Taifa Stars kwenda nchini, Algeria kwa mchezo utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu.
Katibu wa Kamati ya Timu ya Taifa Stars, Teddy Mapunda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu timu hiyo kwenda nchini Algeria kushiriki  mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 17  mwaka huu. Kampuni ya Ndege ya Fastjet imedhamini safari hiyo kwa kutoa ndege yake kwa kwenda na kurudi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati na Kushoto ni Mkuu wa Masoko wa Fastjet, Jan Petrie.
 Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (katikati),akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kudhamini timu ya Taifa Stars kwenda na kurudi  nchini Algeria kwa ndege yake kushiriki  mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 17  mwaka huu. Kulia ni Katibu wa Kamati ya Timu ya Taifa Stars, Teddy Mapunda na Mkuu wa Masoko wa Fastjet, Jan Petrie. 
 Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Ndege ya Fastjet imetoa ndege kwa ajili ya kuisafirisha timu ya Taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wake na timu ya Taifa ya nchi hiyo.Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi  Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati alisema hatua ya kuisaidia timu hiyo ni mwanzotu wa ushirikiano baina ya kampuni hiyo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

“Kampuni yetu imeanza ushirikiano na TFF katika kukuza michezo nchini na ndio maana tumeanza kuwasafirisha wachezaji hao kwenda nchini humo kwa ajili ya mchezo huo” alisema KibatiKatibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda alisema safari ya kwenda nchini humo itakuwa Novemba 16 na kuwa mchezo huo utafanyika Novemba 17.

Alisema gharama za kusafiri na timu hiyo kwa mtu atakayependa kusafiri ni dola 800 kati ya hizo dola 640 ni kwa ajili ya safari na 60 ni malipo ya kodi ya uwanja wa ndege hapa nchini na Algeria.

Alisema safari hiyo itaanza asubuhi na kuwa ndege hiyo watakayosafiri nayo inabeba abiria zaidi ya 150.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)


Loading...

Toa comment