The House of Favourite Newspapers

Faulo Zampasua Kichwa Nabi

0

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amekuwa akipasua kichwa namna ya kuweza kutatua tatizo la mabao ya mipira iliyokufa jambo ambalo limekuwa tatizo kwa timu hiyo kwa hivi karibuni.

 

Kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Rivers United v Yanga uliopigwa juzi nchini Nigeria na Yanga kupigwa bao 1-0, safu ya ulinzi pamoja na viungo wa Yanga wamekaa kikao ili kujadili namna ya kuweza kuondoa hali hiyo.

 

Taarifa kutoka kwa moja ya viongozi wa Yanga ilieleza kuwa Nabi hafurahishwi na kuona timu hiyo inafungwa mabao yanayotokana na mipira ya kutengwa jambo ambalo linampasua kichwa.

 

“Baada ya mchezo dhidi ya Rivers United lile bao lilifanya Nabi aweze kukaa na wachezaji na kuzungumza nao kuhusu makosa ya mara kwa mara, kikubwa anahitaji umakini na hilo litakuwa na mabadiliko makubwa,” alisema mtoa taarifa hiyo.

 

Moja ya mabeki wa kutegemewa ndani ya Yanga ambaye ni nahodha, Bakari Mwamnyeto alisema kuwa kumekuwa na tatizo katika mabao wanayofungwa kutokana na mipira ya kutengwa jambo wanalolinfanyia kazi ili lisijirudie. 

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply