Kartra

FC Platinum Yamtaka Luis Miquissone

DENZIL Mkandla, meneja wa wachezaji wa Klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe amesema kuwa mpango mkubwa wa kwanza katika usajili ni kupata saini ya Luis Miquissone anayekipiga ndani ya Simba.

 

 

Mkandla ameweka wazi kuwa Luis ni mchezaji wa kipekee ndani ya uwanja kwa kuwa anaonyesha kiwango cha hali ya juu muda wote.

 

 

FC Platinum ilitolewa na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kukubali kichapo cha mabao 4-0 Uwanja wa Mkapa ila ule mchezo wa Kwanza, Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe ilishinda bao 1-0.

 

 

Mfungaji wa bao la FC Platinum, Perfect Chikwende kwa sasa yupo ndani ya Simba akiwa ni maalumu kwa michezo ya ndani ambapo ameshaanza kucheza mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.


Toa comment