The House of Favourite Newspapers

Fedha za Maadhimisho ya Uhuru Kujenga Mabweni ya Shule Nane

0

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akizungumza na waandishi wa Habari Katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mjini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema fedha zilizokuwa zimetengwa na Wizara na Taasisi kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru mwaka huu zitapelekwe Ofisi ya Rais – TAMISEMI nakutumika kujenga mabweni katika shule nane za Msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum hapa nchini.

Taarifa hiyo na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Dodoma.

“Shilingi Milioni 960,000,000/- (Tshs Milioni Mia Tisa Sitini)  zitatumika kujenga shule ya msingi Buhangija Shinyanga, Goweko Tabora, Darajani Singida, Mtanga Lindi, Songambele Lindi, Msanzi Rukwa,  Idofi Njombe, na Longido Arusha.”

Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakiwa katika Mkutano.

 

Ni dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Rais wetu ya kuwajali na kuwajengea mazingira rafiki watu wenye mahitaji maalum hapa nchini. Hili ni jambo kubwa la kishujaa na la kupongezwa sana na Wananchi wote wa Tanzania.

Aidha Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka huu 2022 yatafanyika kwa Midahalo na Makongamano mbalimbali yatakayofanyika katika Wilaya zote hapa nchini kujadili, kutafakari kwa pamoja na kukumbuka tulikotoka, tulipo na tunakoelekea kuhusu Maendeleo Endelevu ambayo Nchi yetu adhimu Tanzania imeyafikia. Hivyo hakutakuwa na Gwaride na shughuli nyingine za Kitaifa.

Waziri amesema, Maadhimisho ya MIAKA 61 YA UHURU yataadhimishwa kwa Kauli mbiu inayosema  “AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU”.

“Makongamano hayo yatatanguliwa na ratiba mbalimbali kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya kufanya shughuli za Kijamii kama vile kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali, shule, nyumba za Wazee na makundi yenye mahitaji maalum”

Waziri ameelekeza Ofisi zote za Serikali hapa nchini kupambwa kwa mapambo ya rangi za Bendera ya Taifa pamoja na picha ya Mheshimiwa Rais.

Leave A Reply