The House of Favourite Newspapers

Fei Toto Aweka Rekodi Yanga

0

KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameweka rekodi ndani ya Yanga mara baada ya kufanikiwa kuiongoza timu hiyo kushinda michezo miwili mfululizo ya ligi kuu akiwa kama nahodha wa kikosi hicho.

Tangu ajiunge na Yanga mwaka 2018, Fei Toto hakuwahi kuwa nahodha wa Yanga katika mechi za kimashindano walizocheza.

Msimu huu wakati nahodha mkuu Bakari Mwamnyeto akiwa majeruhi, Fei Toto amekiongoza kikosi hicho katika michezo dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold ambayo yote Yanga imeshinda kwa bao 1-0, huku Fei Toto akifunga bao moja la ushindi dhidi ya Kagera Sugar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Fei Toto alisema anafurahia kuona amefanikiwa kuiongoza Yanga kushinda michezo hiyo akiwa kama nahodha, huku akiweka wazi kuwa bila nguvu ya wachezaji wengine hilo lisingekamilika.

“Nashukuru kwa kuwa ni jambo jema, sikuwahi kufikiria hili lakini kwa kuwa limetokea tumeshinda michezo yote miwili nikiwa kama nahodha, nashukuru sana.

“Hii ni maana halisi ya kuwa na ushirikiano kwani peke yangu nisingeweza kufanikisha ushindi tulioupata, tulishirikiana vema wachezaji, waalimu na mashabiki waliojitokeza kutupa hamasa ya kushinda, tukafanikiwa,” alisema Fei Toto.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

Leave A Reply